Kisumo: Mbowe acha kuitumbukiza nchi yetu kwenye uvunjifu wa amani
Moshi. Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo, amemvaa Mwenyekiti wa
Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe akimtaka aache kile alichodai ni
kuitumbukiza nchi kwenye machafuko.
“Unaposema huna imani na
JWTZ, huna imani na Polisi wetu unataka kuanzisha vikundi vya kukulinda
tafsiri yake ni kwamba unataka kuanzisha vikundi vyenye sare hii si sahihi,” alisema.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kisumo alisema kauli ya Mbowe
inamaanisha anataka kupata msaada wa vijana wake kufundishwa kumlinda
yeye na kuhoji ni nchi gani inafadhili chokochoko hizo.
“Zipo
nchi zina mapesa mengi na zipo tayari kufadhili machafuko nchi nyingine
lakini nchi zilizostaarabika kama Ujerumani, Marekani, Uingereza na
nyingine haziwezi kujiingiza huko,” alisema.
Alisema anaamini
hata Ujerumani ambayo imekuwa ikikifadhili Chadema, haitakubali kutoa
fedha kufadhili uanzishwaji wa vikundi hivyo vya ulinzi wakati vyombo
halali vya ulinzi ni Polisi na JWTZ.
Kisumo alifafanua kuwa
vyama vya siasa vina sare zake na kusema CCM, Chadema na Cuf navyo vina
sare lakini kutaka kuanzisha vikundi vya ulinzi inamaanisha vitapaswa
kuwa na sare za kijeshi.
Kwa mujibu wa Kisumo, anaamini
vyombo vya ulinzi na usalama nchini havitaruhusu kutekelezwa kwa mpango
huo kwani unalenga kuwachochea wafuasi wa Chadema kutokutii mamlaka ya
dola.
Suala la Chadema kutangaza mpango wake wa kuanzisha
vikundi vya ulinzi limeibua mjadala mkali kati yake na CCM ambacho
kinamiliki kikundi cha Green Guard huku Chadema wakimiliki Red Brigade.
CHANZO JUMA MTANDA BLOG
Kisumo: Mbowe acha kuitumbukiza nchi yetu kwenye uvunjifu wa amani
Moshi. Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo, amemvaa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe akimtaka aache kile alichodai ni kuitumbukiza nchi kwenye machafuko.
“Unaposema huna imani na JWTZ, huna imani na Polisi wetu unataka kuanzisha vikundi vya kukulinda tafsiri yake ni kwamba unataka kuanzisha vikundi vyenye sare hii si sahihi,” alisema.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kisumo alisema kauli ya Mbowe inamaanisha anataka kupata msaada wa vijana wake kufundishwa kumlinda yeye na kuhoji ni nchi gani inafadhili chokochoko hizo.
“Zipo nchi zina mapesa mengi na zipo tayari kufadhili machafuko nchi nyingine lakini nchi zilizostaarabika kama Ujerumani, Marekani, Uingereza na nyingine haziwezi kujiingiza huko,” alisema.
Alisema anaamini hata Ujerumani ambayo imekuwa ikikifadhili Chadema, haitakubali kutoa fedha kufadhili uanzishwaji wa vikundi hivyo vya ulinzi wakati vyombo halali vya ulinzi ni Polisi na JWTZ.
Kisumo alifafanua kuwa vyama vya siasa vina sare zake na kusema CCM, Chadema na Cuf navyo vina sare lakini kutaka kuanzisha vikundi vya ulinzi inamaanisha vitapaswa kuwa na sare za kijeshi.
Kwa mujibu wa Kisumo, anaamini vyombo vya ulinzi na usalama nchini havitaruhusu kutekelezwa kwa mpango huo kwani unalenga kuwachochea wafuasi wa Chadema kutokutii mamlaka ya dola.
Suala la Chadema kutangaza mpango wake wa kuanzisha vikundi vya ulinzi limeibua mjadala mkali kati yake na CCM ambacho kinamiliki kikundi cha Green Guard huku Chadema wakimiliki Red Brigade.

1 comments:
KWAHIYO MZEE KISUMO UNAFURAHIA MIKUTANO YA CHADEMA INAFANYIWA UNYAMA?
Post a Comment