Jeshi
la polisi mkoani Kilimanjaro linamhoji mkazi mmoja wa mjini Moshi kufuatia kisa
cha mtoto wake kutoweka nyumbani na silaha anayoimiliki kihalali.
Bwana Antony Justine mkazi wa kiboroloni mjini Moshi ambaye
ni ni mmilikiki halali wa silaha aina ya bastola yenye nambari PA 21738 V
anadaiwa kuhifadhi silaha hiyo kizembe kiasi cha kusababisha mtoto
wake kuiba silaha hiyo.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Roberty Boaz amesema
katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa silaha hiyo ilichukuliwa na
mtoto wa familia ya Bwana Antony aitwaye Melkzedeck 23.
Mtoto huyo alichukua silaha hiyo na vifaa vingine kisha
kuisalimisha kwa polisi baada ya kutoa shinikizo kuwa asibughudhiwe vinginevyo
atajiua kwa kutumia silaha hiyo.
Hata hivyo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wasamaria
wema limefanikiwa kuioka silaha hiyo kutoka mikononi kwa kijana huyo lakini
halikufanikiwa kumkamata kwani aliiacha silaha kichakani na kutokomea
kusikojulikana.
Kisa hicho bado kinaumiza vichwa vya maafisa wa polisi na
hadi sasa uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika kubaini chanzo cha tukio hilo.
Kamanda Boaz amesema jeshi la polisi limetoa onyo kali kwa
mmliki wa silaha hiyo bwana Antony kwa uzembe wa kuhifadhi basatola yake huku
likitoa mwito kwa wamiliki wengine wa silaha kuwa makini katika utunzaji wake
vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
0 comments:
Post a Comment