Kampuni
ya Tanzania Mwandi ikishirikiana na Majimaji FC, imeandaa mkutano wa
wadau wote wa soka mkoani Ruvuma chini ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.
Said Mwambungu, mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Centenary tarehe
10. 08. 2013, kuanzia saa 2 asubuhi.
Lengo
kubwa la mkutano ni kurejesha makali ya 1985, 1986 na 1998 kwa klabu ya
soka ya Majimaji kwa kuiunda upya kiuchumi chini ya mfumo wa Kampuni,
kuijengea uwezo wa kimkakati na kiuendeshaji ili iweze kushiriki kwa
mafanikio Ligi Daraja la Kwanza na hatimaye kurejea Ligi Kuu msimu
ujao.Itakumbukwa kuwa Majimaji FC ni klabu ambayo imezalisha magwiji
wengi wa soka Tanzania kama Abdala Kibadeni ‘Mputa’,
Madaraka
Suleimani ‘Mzee wa Kiminyio’, Peter Tino, Steven Mapunda ‘Garincha’,
Hamis Gaga, Idd Pazi, Omary Hussein ‘Machinga’ na Mdachi Kombo na ni
klabu ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa kwa Simba na Yanga.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Mwandi, Bwana Teonas Aswile amewaalika
wafadhili na wadau wote wenye mapenzi mema na Majimaji FC kujitokeza na
kushiriki katika zoezi la mjadala wa muundo mpya wa Majimaji na hata
kununua hisa kwani sasa Majimaji Kampuni haitakuwa na longolongo zozote.
“Binafsi
nawahimiza wafadhili wa soka kwamba hii ni fursa adimu nyingine ya
kuwekeza fedha zao mahali salama. Majimaji itakuwa ikiendeshwa kikampuni
na miradi mbalimbali itaanzishwa na klabu ikiwemo upande wa ukandarasi
na kuuza wachezaji nje ya nchi. Kwahiyo atakayenunua hisa atafaidika
mara mbili.” alisema Teonas Aswile.
Akizungumziawachokoza
mada wakuu wa Majimaji Revival Conference, Aswile amesema kuwa Wakala
wa Kimataifa wa FIFA na Mwanasheria Maarufu nchini, Dkt Damas Ndumbaro
pamoja na Bwana Silas Mwakibinga, mhasibu na mdau mkubwa wa michezo
ambaye ameshashika nafasi mbalimbali.
Kwa
sasa maandalizi kwaajili ya Mkutano wa Wadau wa Majimaji FC
“Wanalizombe” yanaendelea vyema na wanaohitaji taarifa wanaweza
kuwasiliana na Bwana Nasib Mahinya kwa 0655 468800.Pia viongozi wa
Majimaji FC kama Katibu Mkuu Majimaji FC 0752 622887
0 comments:
Post a Comment