Home » » JE WAJUA HAYA?: MARANGU ENEO LENYE MAJI YENYE MAAJABU

JE WAJUA HAYA?: MARANGU ENEO LENYE MAJI YENYE MAAJABU



Kihistoria jina Marangu linatokana na neno Morangu neno la kichaga cha zamani kabla ya kuchakachuliwa na usasa,maana halisi ya neno hili ni nchi yenye maji mengi.

Kwa wageni wanaofika eneo hili ambalo lipo kwenye mitelemko ya mlima Mashariki kitu cha kwanza kukiona ni msitu mzito wa migomba na miti,cha pili ni madaraja yasio na idadi yanapita juu ya mito na chemichemi nyingi zilizopo eneo hili ambapo pia ni makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

Moja ya maeneo yenye maajabu ni kijiji cha Ashira ambacho ni maarufu kutokana na kuwa karibu na Shule ya Sekondari ya Ashira ambayo kwa miaka mingi mamia na mamia ya wataalamu wamepitia hapa.Ndani ya kijiji hiki kuna msitu mkubwa uitwao Yenunyi ambao ni chanzo kikubwa sana cha maji kwani kuna chemichemi nyingi zinazoanzia hapa.Maji ya chemichemi hizi ni meupe na matamu na husambazwa kwa mfumo wa mabomba na mifereji kwenda kwenye taasisi na vijiji vyote vya karibu.

Katikati ya msitu huu ndipo yalipokuwa makazi ya Mkuu wa ukoo wa Mtui aliyeitwa Kimori.Huyu aliishi wakati ule koo mbalimbali zilikuwa zinapigana ilikuweza kupata ukoo wenye nguvu kuunda utawala yaani Umangi.

 

 ENDELEA KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa