Moshi.Serikali inadaiwa kupoteza mamilioni ya
fedha katika mapato ya uuzwaji viwanja kutokana na udanganyifu
unaofanywa na wauzaji, pamoja na wanunuzi wa mkoani Kilimanjaro .
Imebainika kuwa viwanja vingi vinavyouzwa ama kununuliwa mkoani hapa havilipiwi kodi.
Mbali na baadhi ya mawakili wasio waaminifu
kuandaa mikataba miwili, miwili lakini baadhi ya viwanja vimeuzwa na
wamiliki wake kuficha taarifa halisi za thamani ama bei iliyotumika
kuuza viwanja hivyo.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa, taarifa za uthamini
wa majengo na viwanja hupotoshwa kwa makusudi na baadhi ya wathamini
wanaotambulika ili kuwawezesha wauzaji kukwepa kodi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa
Kilimanjaro,Patience Minga alisema mamlaka yake imeandaa utaratibu wa
kuwazawadia wananchi watakaofichua mauzo ya aina hiyo.
“Tuna fedha kwa hiyo kama kuna mtu atatuletea
taarifa ya aina hiyo atapata kamisheni lakini tumeshaweka utaratibu wa
kutoruhusu kuhamisha umiliki kabla kodi haijalipwa,”alisisitiza Minga.
Kwa mujibu wa Minga, hata kama watadanganya kuhusu
bei halisi ya mauzo,lakini wanapotaka kuhamisha umiliki TRA itafanya
hesabu za kodi kwa kuzingatia bei ya soko na siyo mikataba.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment