Marangu.Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali
George Waitara, jana amepokea ujumbe wa maofisa wa Jeshi la Wananchi
(JWTZ) na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini(TTB), Balozi Charles Sanga
baada ya kumaliza kupanda Mlima Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Maafisa hao wa Jeshi, pamoja na watendaji wa Bodi
ya Utalii, walianza kupanda mlima huo, mrefu barani Afrika Desemba 6
mwaka huu na baadhi kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru na kusimika
Bendera ya Taifa.
Akizungumza wakati wa kupokea ujumbe huo, Waitara
ambaye ndiye muasisi wa mpango huo, uliopewa jina la Uhuru Expedition,
alisema lengo la mpango huo pia ni kuhamasisha utalii wa ndani.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment