WATUHUMIWA watatu raia wa kigeni wa kusafirisha dawa za kulevya
jana wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kusomewa
mashtaka matatu tofauti.
Watuhumiwa hao ni Grace Teta Gratu(24) Liberaia, Josian Dede Crepy(25) Togo na Julius Nyaoro raia wa Kenya.
Mbele ya Hakimu Mkazi Moshi Simon Kobelo, Mwendesha Mashtaka wakili
wa serikali, Janet Sekule, alidai kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa
nyakati tofauti katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA).
Mwendesha Mashtaka, Patrick Mwita akisaidiana na Sekule, aliieleza
mahakama kuwa Josian na Julius katika vipindi viwili tofauti kati ya
Novemba na Desemba, walikula njama na kusafirisha dawa za kulevya
kinyume na sheria.
Katika kosa la pili, Mwita alieleza kuwa washtakiwa hao wanashtakiwa
kwa kosa la kusafirisha kilo 2.2 ya dawa za kulevya aina ya Heroine,
zenye thamani ya sh milioni 88.
Kwa upange wa Grace, Mwendesha Mashtaka alidai kuwa alikamatwa
akiwa na kilo 10.5 za Cacaine zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 100.
Washtakiwa hao walikana makosa na kesi hiyo itakuja kutajwa tena Desemba 24 mwaka huu.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment