Home » » MOSHI WAPANGA KUTUMIA SH.57 BILIONI 2014/2015

MOSHI WAPANGA KUTUMIA SH.57 BILIONI 2014/2015

Moshi.Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, imekusudia kutumia Sh57.35 bilioni katika Mwaka wa Fedha 2014/15 kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Akisoma taarifa kuhusu bajeti katika kikao cha Baraza la Madiwani, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Fulgence Mponji, alisema fedha hizo zitatokana na vyanzo vya ndani vya halmashauri.
Alitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na ada za shule, mifuko ya afya ya jamii, fidia ya kodi, ruzuku ya mishahara, ruzuku ya matumizi na miradi mingine ya maendeleo.
“Kweli tukisimamia mapato yetu ya vizuri na kwa utaratibu uliopo, lazima tutapata fedha hizi na tunaweza kufikia malengo ya bajeti hii,”alisema Mponji.
Alisema katika ruzuku ya mishaara halmashauri hiyo inatarajia Sh43.38 bilioni na ruzuku ya matumizi Sh4.10 bilioni.
Alisema kiasi kingine cha Sh 6.88 bilioni, kitatokana na vyanzo vya halmashauri.
Aliongeza katika mifuko wa afya ya jamii, halmashauri inakusudia kukusanya zaidi ya Sh209 milioni wakati , ada za shuleza sekondari zitakuwa Sh604 milioni na fidia ya kodi Sh499 milioni.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Moris Makoi,aliwataka watendaji kuhakikisha kuwa miradi iliyopangwa inatekelezwa ipasavyo.
Alisema kufanya hivyo, kutawafanya wananchi kuwa na imani zaidi na halmashauri yao hasa kuhusu matumizi ya fedha za umma ambazo mara nyingi zinalalamikiwa.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa