Home » » MBUNGE AWAASA MADIWANI KUSIMAMIA MIRADI

MBUNGE AWAASA MADIWANI KUSIMAMIA MIRADI

Betty Machangu, Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro
 
Madiwani na viongozi wengine katika halmashauri ya Moshi Vijijini wametakiwa kusimamia kikamilifu miradi inayotolewa na halimashauri pamoja na serikali kuu.
Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Betty Machangu, alisema kumekuwa na usimamizi mdogo wa miradi vijijini kutokana na uzembe wa madiwani na viongozi wa kata ambao wanatakiwa kusimamia na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.

Alisema halmashauri inajitahidi kukusanya fedha ambazo kwa mwaka zinafikia Sh. bilioni mbili, lakini zinapopelekwa katika miradi kwa wananchi, viongozi wa kata wanashindwa kusimamia ipasavyo ili fedha zifanye kazi iliyokusudiwa.

“Viongozi wa kata kazi yao kubwa ni kusikiliza kero za wananchi na kuhakikisha kero zinapatiwa ufumbuzi kwa sababu wanaishi ngazi za chini,” alisema Machangu.

Machangu alisema wanasiasa ni lazima wajue kuwa kuna wakati wa kuwatumikia wananchi na wakati wa kampeni za kisiasa. 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa