MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Moshi (MUWSA) imeanzisha kitengo cha
mfumo wa kijiografia (GIS) kitakachokuwa na jukumu la kukusanya taarifa
za wateja wa maji na kuzihifadhi katika mfumo wa kielektroniki ili
kuwezesha utoaji wa huduma sahihi.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mchambuzi wa mfumo huo wa mamlaka
hiyo, Idd Semkunde, alisema kuanzishwa kwa utaratibu huo ni sehemu ya
mipango ya mamlaka hiyo kujiendeleza, ili kuweza kutoa huduma kwa
wateja wake walioko katika mji wa Moshi na maeneo mengine inayohudumia.
Alisema mfumo huo utasaidia kuwatambua wateja wote wa mamlaka pamoja
na taarifa zao, ili kuwa karibu pindi panapotokea tatizo katika
miundombinu ya mamlaka hiyo pamoja na urahisi wa kupeana taarifa kwa
njia ya simu ya mkononi.
Semkunde alisema katika kuhakikisha utaratibu huo unafanikiwa,
mamlaka inafanya mawasiliano na serikali za mitaa, ili kuzungumza na
wananchi wao waweze kutoa taarifa sahihi kwa watumishi wa mamlaka
watakaopita kukusanya taarifa hizo.
“Huu ni utaratibu mpya kwa MUWSA lakini pia kwa watu wa Moshi na
maeneo mengine yanayohudumiwa na Muwsa, tunaomba wananchi watupe
ushirikiano pindi maofisa wa mamlaka wanapofika majumbani mwao, kwani
mwisho wa zoezi tunachukua namba za simu kwa sababu baadaye wateja wote
wanaohudumiwa na Muwsa watakuwa wanapokea taarifa kwa njia ya simu,”
alisema Semkunde.
Alisema mfumo wa kielektroniki wa utunzaji taarifa utakapokuwa
umeandaliwa vema mamlaka itakuwa kwenye kiwango ambacho mteja hatakuwa
na haja ya kupanga foleni kulipia ankara
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment