Moshi. Kamatakamata ya watu wanaoshukiwa kuiba mabomba ya maji
nyumbani kwa Waziri mkuu mstaafu, Cleopa Msuya, imeibua malalamiko
miongoni mwa wakazi wa Wilaya ya Mwanga.
Mabomba hayo 80, yanadaiwa kuwa na thamani ya
Sh2,485,000 na tayari watu sita wamefikishwa mahakamani kwa nyakati
tofauti wakihusishwa na tukio hilo.
Takribani watu 30 wamekamatwa na kuhojiwa tangu
uchunguzi ulipoanza, baadhi ya watuhumiwa wakiwatuhumu baadhi ya polisi
wasiokuwa waaminifu kuomba rushwa ya hadi Sh500,000 ili wawaachie.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Mbunge wa Mwanga
ambaye pia ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, alisema hata
yeye amelifahamu juzi.“Kuna wananchi wengi wakiwa ni vijana wamekuja na
kulalamika kuwa kuna operesheni inayowaletea usumbufu mkubwa watu
wasiohusika na huo wizi,”alisema mbunge huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa ni Kilimanjaro, Robert
Boaz, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo nyumbani kwa Msuya na
kutahadharisha uchunguzi huo usipotoshwe kwa sababu zozote zikiwamo za
kisiasa.
“Uchunguzi wowote wa kipolisi unaweza kugusa watu
mbalimbali, tusiibue malalamiko yasiyokuwa na ushahidi ili haki
isitendeke, uchunguzi ni wa kijinai lazima washukiwa wahojiwe, ”alisema.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment