Home » » Watakiwa kusaidia wahanga

Watakiwa kusaidia wahanga

Hai. Katibu Tarafa wa wilayani hapa, Nsajigwa Udagile amewataka wanakijiji wa Lerai mkoani Kilimanjaro kusaidia waliopatwa na maafa yaliyotokea kijijini hapa, yaliyosababishwa na upepo mkali na kimbunga yaliyoezua darasa moja la Shule ya Msingi Lerai.
Katibu Tarafa huyo amezungumza hayo katika mkutano ulioandaliwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Lerai,Arpakwa Mamasita.
Amesema ni jukumu na wajibu wa kuchangia maafa hayo yaliyotokea hivi karibuni na kuleta hasara kijijini hapa. Alisema bila ushirikiano maendeleo ya wanafunzi yatadumaa.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa