Home » » AJALI MBAYA YATOKEA MWEKA ,MOSHI VIJIJINI YAHUSISHA VX NA DALADALA

AJALI MBAYA YATOKEA MWEKA ,MOSHI VIJIJINI YAHUSISHA VX NA DALADALA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na moshi mjini  na landcruiser VX iliyokuwa  imewabeba  wanafunzi wa chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyama pori Mweka kilichopo Mweka , Moshi vijijini.Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyobwana Fred Mushi amesema kuwa gari aina ya landcruiser VX iligonga daladala  hiyo  iliyo kuwa imesimama kupakia abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. Ajali hiyo imetokea muda wa saa 10.30 jioni ya jana
Gari aina ya landcruiser VX iliyokuwa na wanafunzi toka chuo cha Mweka ikiwa imezama kwenye mtaro  na kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo mbaya iliyotokea jioni ya jana




mashuhuda walikokuwa eneo la tukio wakilitazama gari aina ya landcuriser iliyokuwa imezama kwenye mtaro baada ya ajali hiyo iliyotokea jioni jana na kusababisha majeruhi
daladala iliyogongwa vibaya na landcuriser ikiwa imeharibika vibaya ubavuni kiasi cha kutoweza kutembea tena lakini Taarifa za awali hali ya dereva wake   inasemekana kuwa mbaya pia idadi ya majeruhi mpaka tunaenda mitamboni  haijajulikana.tutaendelea kukujuza jinsi taarifa zitakavyofikia kuhusu hali na idadi Ya majeruhi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa