Home » » `Igeni moyo wa Dk. Mengi kutoa misaada kwa jamii`

`Igeni moyo wa Dk. Mengi kutoa misaada kwa jamii`

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi.
 
Wafanyabiashara  nchini wametakiwa kuiga moyo wa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, wa kutoa misaada kwa jamii na vikundi vya wajasiriamali nchini.
Rai hiyo ilitolewa na Meneja wa Hoteli ya Continental ya jijini Dar es Salaam, Betul Chove, wakati akikabidhi msaada wa Shilingi milioni tatu kwa kikundi cha Kiandiko Group cha mkoani Kilimanjaro.

“Kutoa msaada katika vikundi ni mkakati wa hoteli yetu ambao tulijiwekea, ”alisema Chove na kuongeza:  “Ni muhimu tukaungana na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk.

Reginald Mengi, katika kuwasaidia wajasiriamali kwani amekuwa mstari wa mbele katika hili na watu na si kwa sababu ni tajiri hapana, ni moyo aliokuwa nao."

Chove alisema kuna wafanyabiashara wengi nchini lakini hawana  moyo wa kujitolea kusaidia wengine wanyonge kama ilivyo kwa Dk. Mengi. 

Akipokea msaada huo, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Ramadhani Mlawa, aliuhushukuru uongozi wa hoteli hiyo na kutaka wafanyabiashara wengine kuiga mfano huo.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa