Familia za zaidi ya watu 300 zimenusurika vifo wilayani Mwanga
baada ya mvua iliyoambatana na upepo kuezua mapaa ya nyumba zao 110 .
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu Ndemanga aliliambia gazeti hili jana kuwa hali katika eneo hilo ni mbaya.
Ndemanga alisema mvua hiyo ilinyesha juzi kati ya
saa 10:30 na saa 11:30 jioni na kuezua mapaa ya nyumba hizo katika Kata
mbili za Mwaniko na Kifula.
“Upepo hasa ulioleta madhara ulivuma kwa dakika
kama tano tu hivi japo mvua ya upepo ilinyesha kwa saa moja.... Nimetoka
huko hali ni mbaya,”alisema.
Ndemanga alisema upepo huo uliezua paa za nyumba
44 katika Kata ya Mwaniko na nyumba 64 katika Kata ya Kifula huku maelfu
ya ekari za migomba zikiwa zimeathiriwa vibaya.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, upepo huo
umeezua mapaa ya madarasa saba ya Shule ya Msingi Mangio, ofisi ya
walimu na choo cha wanafunzi.
“Kutokana na athari za maafa hayo ni wanafunzi wa
darasa la saba, sita na nne tu ndio watakaoendelea na masomo na wengine
watabaki nyumbani,”alisema.
Ndemanga alifafanua kuwa, leo wataalamu wa ujenzi
watapiga kambi katika shule hiyo kuhakikisha inarejea katika hali yake
ya kawaida ndani ya siku saba.
Alisema familia ambazo zimekumbwa na maafa hayo
zenye watu wasiopungua 300 zimepatiwa hifadhi na ndugu wakati serikali
ikiwa katika harakati za kufanya tathmini ya haraka ili kubaini
uharibifu huo..
“Ni hali ya kutisha, lakini mpaka sasa hakuna
taarifa za vifo licha ya nyumba mbili kubomoka kabisa....kwa kweli
tunamshukuru Mungu kuwa hakuna madhara zaidi ambayo yamejitokeza hadi
sasa,” alisema.
Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa
Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo ametuma salamu za pole kwa waathirika
wa maafa hayo yaliyotokana na mvua kubwa .
Ndesamburo ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Mjini,
kupitia Chadema, leo atafanya ziara katika wilaya hiyo ambapo pamoja na
mambo mengine kujionea athari za maafa hayo.
“Kesho (leo) Ndesamburo atafika Mwanga na baada ya kujionea hali halisi ndio atatoa tamko rasmi” alisema Basil Lema, Katibu wa Chadema mkoa
Chanzo;Mwananchi
“Kesho (leo) Ndesamburo atafika Mwanga na baada ya kujionea hali halisi ndio atatoa tamko rasmi” alisema Basil Lema, Katibu wa Chadema mkoa
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment