Home » » Waziri Chikawe kufungua mkutano wa vigogo Polisi

Waziri Chikawe kufungua mkutano wa vigogo Polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, leo atafungua mkutano wa siku sita wa viongozi wa juu wa Jeshi la Polisi.
Mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na  Inspekta wa Jenerali (IGP), Ernest Mangu, pia utawashirikisha makamishna, manaibu makamishna waandamizi, makanishna wasaidizi na  makamanda wa mikoa, utajadili masuala mbalimbali yanayolikabili jeshi hilo.

Mkutano huo, unaofanyika mara moja kila mwaka, unawakutanisha watendaji wa juu wa jeshi la Polisi nchini katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (MPA) Mjini Moshi ambao pamoja na mambo mengine ni maalumu kwa ajili ya kujadili mustakabali wa kiutendaji, ndani ya jeshi hilo na namna ya kuongeza ufanisi wa jeshi katika usalama wa raia na mali zao.

Taarifa iliyopatikana jana mjini hapa kutoka kwa Mkuu wa chuo hicho, Kamishna Mwandamizi, Matanga Mbushi, kuhusiana na ujio wa viongozi hao wa kitaifa, inaeleza kwamba mkutano huo unaanza leo na Waziri  Chikawe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

”Ingawa msemaji wa Polisi yupo (Advera Senso) na atawapa taarifa, mimi nafanya tu maandalizi ya ujio wa viongozi mbalimbali ,” Matanga.

Hadi jana mchana NIPASHE ilishuhudia magari kadhaa ya Makamanda wa Polisi wa mikoa mbalimbali nchini wakiwasili mjini hapa.
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa