Home » » Diamond, Joh Makini wapagawisha Moshi

Diamond, Joh Makini wapagawisha Moshi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwishoni mwa wiki alikonga nyoyo za wakazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro, alipotumbuiza katika tamasha la wazi la ‘Good Time ya Ukweli’ lililoandaliwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola.
Wengine waliopanda jukwaani katika tamasha hilo ni mwanamuziki maarufu wa hip hop nchini, Joh Makini ‘Mwamba wa Kaskazini’ na Jambo Squad ambao wanatamba na kibao cha ‘Tukunyema’.
Diamond, aliwapagawisha wakazi wa Moshi alipopanda na kibao chake cha ‘My Number One’ huku  kwa upande wa Joh Makini, akikonga nyoyo za wakazi hao kwa wimbo wake ‘Tatizo ni Bei ya Mkaa’.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Masoko wa Coca-Cola Bonite, Christopher Loiruk, alisema kuwa, ana furaha kwa wakazi wa Moshi kujitokeza kwa wingi katika tamasha la ‘Good Time ya Ukweli na Coca-Cola’ na kwamba, lengo la tamasha hilo ni kutoa burudani kwa vijana na kutoa fursa kufurahi pamoja wakipata viburudisho vya Coca-Cola.
Wakazi wa Mbeya walijimwaga Machi 8 viwanja vya CCM Ilomba na kupata burudani kutoka kwa Wanaume TMK wanaosifika kwa kuimba na kucheza kwa nguvu wanapokuwa jukwaani, ambako mamia ya vijana walijitokeza kwa wingi kupata burudani hiyo.
Mfululizo wa burudani hizo utahitimishwa Machi 23 katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam, ambako wasanii Diamond, Vannesa Mdee na wengine wengi watashambulia jukwaa kwa nyakati tofauti kwa lengo la kutoa burudani ya kukata na shoka kwa vijana.
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa