Home » » KIMARO: VICOBA SULUHISHO LA UMASKINI NCHINI

KIMARO: VICOBA SULUHISHO LA UMASKINI NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

ALIYEKUWA  mbunge wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro, ametoa wito kwa wananchi kujiunga kwenye benki za kijamii vijijini (VICOBA) kama njia ya kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.
Kimaro alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na vikundi vya VICOBA kwenye Kijiji cha Kilindini Wilaya ya Moshi Vijijini ambapo aliendesha harambee ya kuchangia kikundi hicho na kupatikana sh 660,000 huku yeye akichangia sh 200,000.
Aliwataka wanavikundi hao kutumia fursa wanazozipata kujiletea maendeleo na kuondokana na dhana ya kulalamika.
Alisema kupitia vikundi hivyo wananchi wengi wataweza kuendesha maisha yao vizuri ikiwamo kusomesha watoto shule.

Chanzo:Tanzania daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa