Home » » Gurjit bingwa mbio za magari Vaisakhi Rally

Gurjit bingwa mbio za magari Vaisakhi Rally

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Gurjit bingwa mbio za magari Vaisakhi RallyDEREVA wa gari namba 2, aina ya Subaru MY 03, Gurjit Dhani akiongozwa na Shameer Yusuf, ameibuka bingwa wa mashindano yaVaisakhi Rally 2014, mbio zilizofanyika mwishoni mwa wiki.
Dhani alifanikiwa kumvua ubingwa huo dereva mkongwe, Gerrad Miller wa Arusha aliyekuwa akiendesha gari namba 1, aina ya Mitsubishi Evo IX, katika mchuano huo mkali wa mizunguko mitano ya umbali wa kilomita 250.
Nafasi ya pili katika mbio hizo, ilishikwa na Gurpal Sandhu aliyekuwa akiongozwa na Absalom Aswani, wakitumia gari
namba 7, aina ya Mitsubishi Evo X.
Mshindi wa nafasi ya tatu, ni Rajpal Dhani, akiongozwa na Surinder Sudle wakiwa na gari namba 4, aina ya Subaru MY 03.
Akizungumza baada ya kutangzwa mshindi, Gurjit ambaye ni dereva chipukizi, alisema furaha yake si kutwaa ubingwa tu, bali kuwashindwa madereva wakongwe akiwemo bingwa wa
mwaka jana, Mzee Gerrad Miller.
Gurjit alisema kiujumla mashindano ya mwaka huu yalikuwa mazuri tofauti na mwaka jana huku changamoto kubwa ni usalama mdogo kwani kwa baadhi ya maeneo, kulikuwa na watu na mifugo iliyokuwa ikiingia barabarani wakati wa mbio.
“Namshukuru Mungu, nimefarijika sana kushinda mbio hizi,
ushindani ulikuwa ni mkubwa, nina furaha sana kumshinda
Miller. Mashindano yalikuwa mazuri sana, ila usalama unapaswa kuzingatiwa barabarani wakati wa mbio,” alisema Dhani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mbio za magari Kilimanjaro (KMSC), Faheem Aloo, alisema mbio hizo ni faraja sana kwani changamoto zilikuwa nyingi na kuahidi kuziboresha zaidi mwakani.
Naye Mgeni rasmi, Ofisa Michezo Mkoa wa Kilimanjaro, Anthony Ishumi, aliwataka waratibu wa mbio hizo kushirikisha washindani wengi kuifanya michuano hiyo kuwa na sura ya kitaifa.
Katika mbio hizo za mwaka huu, magari yalitakiwa kukimbia
umbali wa kilomita  250 ambapo pia kulikuwa na sehemu ya kilomita nyingine 140 kupitia Miwaleni, Gate Fonga, New Land, Kikavu Chini hadi Kwa Sadala, ambapo sehemu ya matengenezo ilikuwa katika Uwanja wa Meimoria.
Mbio hizo zinazokwenda sambamba na maadhimisho ya sherehe za jamii ya masingasinga, zimedhaminiwa na Umoja wa Masingasinga (Sikh Union).
Chanzo ;tanzania daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa