Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHEHENA ya magunia 300 ya kahawa kutoka Burundi iliyoibwa wakati
ikisafrishwa kutoka nchini humo kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya
Dar es Salaam, imepatikana.
Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki kutoka ndani ya Bodi ya
Kahawa Tanzania (TCB) zimedai kuwa kahawa hiyo imepatikana na bodi
imetuma maofisa wake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi.
Kahawa hiyo ilikuwa ikisafirishwa kwenye lori aina ya Mercedes Benz
lenye namba za usajili A 8564 A na tela lenye namba T 808 BLR liliibwa
karibu na ghala lililopo Barabara ya Nelson Mandela jijini humo Januari
6, mwaka huu.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment