Home » , » WAKENYA WAENDELEA KUTESA KILIMANJARO MARATHON

WAKENYA WAENDELEA KUTESA KILIMANJARO MARATHON

MTANZANIA Jackline Sakilu amewatuliza Watanzania kwa kuibuka mshindi katika mbio za mwaka huu za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon.
Mshindi wa kwanza wa Half Marathoni ,Jackline Sakilu akihitimisha mbio.

Sakilu ambaye anatokea katika Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ), amefanya hivyo jana katika mbio za Kilomita 21 wanawake, akikimbia kwa muda wa saa 1:12:43 mbele ya wanariadha kutoka nchi jirani ya Kenya.

Katika nafasi ya pili alikuwa ni mwanariadha Cynthia Towett, aliyekimbia kwa muda wa saa 1:14:33, na katika nafasi ya tatu alikuwa ni Naomi Maiyo aliyekimbia kwa muda wa saa 1:17:47 wote kutoka Kenya.

Katika mbio hizo kwa upande wa wanaume, nafasi ya kwanza alikuwa ni Alfred Lagat kutoka Kenya ambaye alikimbia kwa muda wa saa 1:02:34 akifuatiwa na Wakenya wenzake Silah Limo (1:03:04) na Keneth Kandie (1:03:20) huku Mtanzania wa pekee katika kumi bora, Alfred Felix, kutoka Klabu ya riadha ya Holili (HYAC) akishika nafasi ya tano (1:03:27).

Wakati huo huo zimwi la kufanya vibaya katika mbio ndefu (Kilomita 42) imeendelea kuiandama Tanzania baada ya Wanariadha kutoka Kenya kutawala mbio hizo kwa mwaka mwengine tena.

Katika Mbio za wanaume, Mshindi  wa  kwanza David Ruto kutoka Kenya aliyetimua mbio hizo kwa muda wa masaa 2:16:04,nafasi ya pili alikuwa ni Julius Kilimo (2:16:17) na nafasi ya tatu ikishikwa na Victor Serem 2:16:32 huku Mtanzania wa kwanza katika mbio hiozo kwa upende wa wanaume, Daudi Lwabe, akiingia katika nafasi ya nane akitumia muda wa masaa 2:18:34.

Katika upande wa wanawake mshindi alikuwa ni Frida Lodera aliyetumia muda wa masaa 2:40:11, nafasi ya pili ni Joan Rotich aliyetumia muda wa masaa 2:42:46 na nafasi ya tatu ikashikwa na Abigal Toroitich ambaye alitumia muda wa masaa 2:55:14 ambapo Mtanzania pekee aliyeingia kumi bora, Banuelia Bryton,  akiingia katika nafasi ya tisa kwa kutumia muda wa masaa 3:12:26.
Kilimanjaro Marathoni imeshirikisha watu wa rika zote.
Mshindi wa kwanza wa Full Marathoni kwa upande wa wanawake Frida Lodepa wa Kenya.
Mbio za Kilimanjaro marathoni zimetuunganisha.
Waliofanikiwa kumaliza mbio walishindwa kusimama na kuhitaji msaada.
Wenye ulemavu pia wameshiriki vyema mbio hizo.
Matibabu yalikuwepo kwa wale waliopata tatizo wakati wa mashindano.

Kampuni ya GAPCO ilisimamia zoezi la zawadi kwa washindi kwa wenye ulemavu.
Kila mwaka huwa kama siku kuu ya kuwakutanisha watu pamoja.
Walemavu wakiwa wamekusanyika baada ya mashindano.
Kawe Jogging club walisafiri toka Dar hadi Moshi kwa ajili ya Kilimanjaro Marathoni.

Wale wa mbio za kujifurahisha Vodacom Fun Run walijinyakulia na zawadi za kutosha toka Vodacom.
Wadau pia walikuwepo.
Waziri wa habari ,utamaduni na Michezo Dk Fenera Mukangara akikabidhi mfano wa hundi ya sh Mil 2 kwa mshindi wa pili wa  Haf Marathoni wanawake.
Washindi wa Half Marathoni wakiwa katika picha ya pamoja.
Mshindi wa kwanza wa Full Marathoni David Ruto akionesha mfano wa hundi ya sh mil 4 iliyotolewa kwa mshindi wa kwanza.
Wadau wakiwa katika maadalizi ya mbio za Vodacom Fun Run.
Msanii wa michezo ya kuigiza Mhogo Mchungu naye pia alikuwa karibu akifuatili mbio hizo. CHANZO: www.kijiwechetu.blogspot.com
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa