Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon
Ndesamburo amewahakikishia wananchi na wafanyabiashara wa Moshi na
vitongoji vyake kwamba soko la mitumba litarejeshwa katika eneo la
Kiborloni.
Ndesamburo alisema kurejeshwa kwa soko hilo kutoka
eneo la muda la Uwanja wa Kumbukumbu ya Mfalme George (Memorial) ni
ahadi ya Chadema waliyoitoa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema
mkoani Kilimanjaro, alitoa kauli hiyo juzi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Kata ya Kiborloni, ambayo ni moja ya ngome za
Chadema.
Ndesamburo alisema baada Chadema ya kupata ridhaa
ya kuongoza halmashauri, azimio la kwanza walilopitisha ni kurejesha
soko hilo lakini mkurugenzi wa wakati huo alikataa kutekeleza azimio
hilo.
Katika hatua nyingine, madiwani watatu, Peter
Kimaro wa Rau, Dk Charles Mmbando wa Soweto na Ovena Kowero wa viti
maalumu, wamesema hawajawahi kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Naibu
Meya.
Nafasi hiyo imeachwa wazi baada ya aliyekuwa akiishikilia, Vicent Rimoy ambaye pia alikuwa Diwani wa Kiborloni, kufariki dunia.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment