Juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa idara ya utalii katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro Eva Mallya |
Na Dixon Busagaga wa Globu
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
HIFADHI
ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ,imetoa fursa kwa wananchi wa Tanzania na
Afrika Mashariki kwa jumla kupanda mlima Kilimanjaro hadi kilele cha
Shira (Shira Plateu) kwa nusu bei yaani shilingi 5,000 kwa watu wazima
kuanzia miaka 16 na kuendelea na Shilingi 1,000 kwa watoto kuanzia miaka
5 hadi 15.
Gharama
hii ni nusu ya bei halisi ambayo ni shilingi 10,000 kwa watu wazima na
2,000 kwa watoto.Ofa hii inaanza Mei 15 hadi Mei 18 mwaka huu,Safari
hiyo itakuwa ya kutwa nzima kwenda na kurudi siku hiyo hiyo na usafiri
utatolewa bure na hifadhi (KINAPA).
Vituo
vya kujiandikishia ni mgahawa wa Fresh coach Moshi mjini ,Hosptal ya
KCMC,Njia Panda ya Himo (Stand ya Same),Bomang’ombe (Kiwire Supermarket)
na KINAPA Marangu(Mapokezi).Kazi ya uandikishaji imeanza tayari.Vituo
vitakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi.Wanaopenda kupanda wanashauriwa
kufika katika maeneo hayo tajwa.
Vituo
vya kuanzia safari ni viwili Mgahawa wa Fresh Coach Moshi mjini na
Bomang’ombe (Kiwire Supermarket),Safari itaanza saa moja kamili asubuhi.
0 comments:
Post a Comment