Home » » MAKURUTA 237 WATIMULIWA KWA KUGUSHI VYETI

MAKURUTA 237 WATIMULIWA KWA KUGUSHI VYETI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Makuruta 237 waliokuwa mafunzoni katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), wamefukuzwa chuoni kwa tuhuma za kughushi vyeti na utovu wa nidhamu.
Waliofukuzwa ni kati ya wanafunzi 3,415 waliosajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Desemba 10 mwaka jana kupata mafunzo hayo.

Mkuu wa Utawala na Masuala ya Utumishi wa Jeshi la Polisi Thobias Andengenye, alisema jana kuwa makuruta hao, walifukuzwa baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), kuiarifu polisi kuwa wameghushi vyeti.

Alisema Necta ilihakiki vyeti vya polisi tarajali 212 na kubaini wameghushi vyeti vya taaluma. Kadhalika alisema wanafunzi wengine  25 kati yao nao walifukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu na matatizo ya kiafya.

Kufuatia hali hiyo, Kamishna Andengenye aliwataka wananchi kuacha tabia ya kugushi vyeti kwa kuwa madhara yake ni makubwa na hatari kwa taifa kutokana na kuhudumia watumishi wasio na sifa iwapo hawatabainika.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limetangaza ofa ya ajira 700 kwa madereva watakaojiunga na jeshi hilo.  Limesema ni lazima waombaji wa nafasi hiyo wapitie chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Andengenye alizitaka taasisi nyingine za umma kuwa makini na watumishi walionao kwa kuwa baadhi yao wanatumia vyeti vya kughushi.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa