Home » » KIWANDA CHA NGOZI HIMO HAKINA HATIMILIKI-WAZIRI

KIWANDA CHA NGOZI HIMO HAKINA HATIMILIKI-WAZIRI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge
 
Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira),  Dk. Binilith Mahenge, amesema Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) halikuweza kufanya tathmini ya mazingira katika kiwanda cha ngozi katika mji mdogo wa Himo, mkoani Kilimanjaro kutokana na kiwanda kutokuwa na hatimiliki.
Alisema mwenye kiwanda hicho hajapewa hatimiliki eneo hilo na hataruhusiwa kuanza shughuli zozote na kwamba anafanya shughuli hizo kinyume cha sheria na kwamba hajapewa tathmini ya athari za mazingira.

“Nimeona ofisini kwangu kiwanda kimeomba kifanyiwe tathmini ya mazingira, lakini watu wangu kupitia NEMC walikwenda ili kifanyiwe tathmini ya mazingira lazima awe na hatimiliki, tumefuatilia na kubaini hakutakiwa kufanya shughuli hizo bila tathmini hiyo,” alisema.

Awali, Mbunge wa Vunjo ( TLP), Augustino Mrema, alisema sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 na sheria ya hifadhi ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na kwamba kiwanda hicho hakikustahili kupata leseni kwa kuwa kinaleta athari za mazingira kwa wakazi wa Mji Mdogo wa Himo.

“Nimeongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mazingira ambaye alisema hajatoa leseni ya mazingira, naomba kauli ya Waziri,” alisema Mrema.

Baada ya majibu hayo, Mrema alisema majibu yanaridhirisha kwa kuwa wananchi walishaanza kukilaumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kwa kuwa mmiliki wa kiwanda hicho alikuwa anatamba ana hati zote wakati siyo kweli.

“Nitakwenda kuwaambia wananchi wangu kuwa haijala kwao, walishaanza kukichafua CCM na serikali yake,” alisema Mrema na kurudisha Shilingi.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa