Home » » WAONGOZA WATALII WAMLILIA RC GAMA

WAONGOZA WATALII WAMLILIA RC GAMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Chama cha Waongoza Watalii Mlima Kilimanjaro na Meru (Kili-Meru) kimemuomba mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama kuwatafutia maeneo ya kilimo katika mikoa mingine ili waweze kujikita zaidi kwenye kilimo badala ya kutegemea kazi ya kuongoza watalii pekee.
Mwenyekiti wa chama hicho, Faustine Chombo alitoa ombi hilo jana wakati wa mkutano mkuu wa chama uliofanyika mjini Moshi. Alisema wakati ambao kunakuwa na msimu wa watalii kidogo, wanakuwa hawana kazi na hivyo wangependa kujihusisha na shughuli nyingine ya kujipatia kipato.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa