Home » » WANAFUNZI 212 WA UASKARI MPA WAACHISHWA MASOMO KWA KUGUSHI VYETI

WANAFUNZI 212 WA UASKARI MPA WAACHISHWA MASOMO KWA KUGUSHI VYETI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


JESHI la polisi nchini, limewafukuza wanafunzi  212 wa uaskari katika
chuo cha taaluma ya polisi Moshi (MPA) kwa kosa kughushi vyeti vya
elimu ya sekondari.
 
Kamishina wa utawala na utumishi wa jeshi la polisi Thobias
Andengenye, aliyabainisha hayo jana wakati wa  mkutano wa waandshi wa
habari pamoja na maafisa wa jeshi hilo katika ukumbi wa mkutano uliopo
katika chuo hicho, uliokuwa na lengo la kutoa taarifa ya wanafunzi wa
uaskari wanaoendelea na mafunzo ya awali  chuoni hapo.
 
Alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na baraza la mitihani la
taifa walifanya zoezi la uhakiki wa vyeti vya wanafunzi hao na ndipo
ilipo bainika kuwa wanafunzi  212 kati ya wanafunzi 3,390 walighushi
vyeti vya elimu ya sekondari.
 
Aidha alisema kufuatia hali hiyo jeshi la polisi nchi limewaachisha
mafunzo ya uaskari wananfunzi hao  ili hatua nyingine za Kiupelelezi
ziendeleee kuchukuliwa kwa kushirikiana na taasisi zingine.
 
Andengenye alisema katika kuhakikisha kwamba jeshi la polisi
linaendela kuwa na askari wenye weledi na uamifu kwa raia na taifa kwa
ujumla, wataelenda kufanya uhakiki  wa vyeti kwa wanafunzi wote ili
kuwabaini wale wote wanao ghushi vyeti.
 
“Itambulike kuwa kitendo chochote cha kughushi ni kosa la jinai na
pindi mtu anapobainika kufanya hivyo jeshi la polisi halitasita
kuwachukulia hatua za kisheria”alisema Andengenye.
 
Andengenye alitumia pia wananchi, kuachana na tabia za kughushi vyeti
au kutumia vyeti ambavyo si vyao,na badala yake wafuate taratibu na
sheria zilizopo kwa ustawi wa taifa letu.
 
Jumla ya wanafunzi 3,415 waliripoti katika chuo cha taaluma ya Polisi
Moshi, Desemba 10 mwaka 2013,ambapo wanafunzi  wa uaskari 25
waliachishwa mafunzo na kubakia wanafunzi 3,390, kutokana na matatizo
ya kiafya na makosa ya Kinidhamu.

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa