Moshi
SIKU chache baada ya mtoto Nasra Rashid kufariki dunia baada ya
kuwekwa kwenye boksi kwa takribani miaka mine, mtoto mwingine wa kike
mwenye umri wa miaka mitano, amefariki duniani huko mkoani
Kilimanjaro, baada ya kubakwa na babake mzazi.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kmanda wa polisi mkoani
Kilimanjaro, Koka Moita, alisema mtoto huyo alifanyiwa unyama huo na
babake aitwae Elisha Wazaeli, (38), huko Mang’ola, wilaya ya Karatu,
mkoani Arusha.
“Kifo cha mtoto huyu ambacho kimewasikitisha watu wengi, kilitokea
Juni 4, mwaka huu katika hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi,
alikokuwa akipata matibabu”, alisema.
Akielezea mazingira ya tukio hilo hadi kufikia kifo cha mtoto huyo,
Kamanda Moita alisema taarifa za awali zilizotolewa kwa jeshi la
polisi zinaonyesha ya kuwa mtuhumiwa alisafiri na mtoto wake huyo hadi
Karatu eneo alilomfanyia unyama huo.
“Alikaa na mtoto huyo huko Karatu kwa siku nne na baada ya kumfanyia
unyama huo, alirudi na mtoto huyo hadi Ngaramtoni, Arusha wanakoishi
lakini baba huyo alitofautiana na mama wa mtoto huyo kabla ya mama
huyo kumchukua mtoto na kwenda nae eneo la Kahe, Moshi, Vijijini, Mkoa
wa Kilimanjaro”, alisema na kuongeza wakati akisafiri na mwanae huyo
kwenda Mang’ola alimwacha mkewe Arusha Mjini.
Alisema kuwa baada ya kufika Kahe mtoto huyo alianza kuugua na
alipopelekwa katika hospitali ya TPC aligundulika anaumwa homa ya
matumbo na kupatiwa tiba na dawa lakini pamoja na tiba hiyo bado
alikuwa akisumbuliwa na maradhi.
“Mama yake alipomchunguza zaidi aliambiwa na mtoto huyo ya kuwa
anaumwa na sehemu zake za siri na alipomhoji zaidi ndipo alipomwambia
ya kuwa babake alimuingilia kimwili wakiwa Karatu,ambapo mamake
alimchunguza sehemu zake za siri na kukuta ameharibika vibaya huku
akitoa harufu mbaya”, alisema.
Alisema mama huyo alitoa taarifa kwa jeshi la polisi ambapo maofisa wa
jeshi hilo walimchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitali ya Mawenzi
kwa uchunguzi zaidi na matibabu hadi alipofariki dunia juzi.
“Ukweli ni kwamba mtoto Yule alipoletwa hapa polisi jana (Juni 4),
alikuwa ameharibika vibaya sehemu zake za siri,kwani alikuwa akitoa
harufu ya kuoza,na baada ya kufika hapa alipelekwa hospitali ya
Mawenzi kwa ajili ya matibabu ambapo alilazwa,lakini alifariki dunia
ilipofika saa Moja usiku”alieleza Kaimu Kamanda Moita.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda, mtuhumiwa wa tukio hilo Elisha Wazaeli,
ametoroka na kwamba tayari jeshi la polisi mkoani humo limeanza msako
wa kumtafuta ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Kaimu Kamanda alitumia nafasi hiyo kuwataka wazazi hususani wakina
mama, kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao, badala ya kuwaachia
wafanyakazi wa nyumbani jukumu hilo muhimu la malezi.
Alisema kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ubakaji kwa watoto
wadogo, ni lazima wazazi wahakikishe wanajijengea tabia ya kuwa karibu
na watoto wao na ikibidi kuwakagua mara kwa mara, hatua ambayo
itasaidia kugundua kwa urahisi pindi mtoto anapofanyiwa vitendo kama
Home »
» HATARI SANA: MTOTO AFARIKI BAADA YA KUBAKWA NA BABAKE MZAZI
HATARI SANA: MTOTO AFARIKI BAADA YA KUBAKWA NA BABAKE MZAZI
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:
Post a Comment