Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeibuka
kidedea katika kesi ya madai ya fidia ya Sh700 milioni iliyokuwa
imefunguliwa dhidi yake na Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu, Peter Jonathan.
Jaji Jonathan ambaye sasa ni wakili wa
kujitegemea, alifungua kesi hiyo mwaka 2008 akidai fidia hiyo kwa madai
ya kudhalilishwa na Takukuru.
Kiini cha kesi hiyo ni kitendo cha Takukuru
kumkamata Jaji huyo Juni 5, mwaka 2007 na kumsweka mahabusu ya Kituo
Kikuu cha Polisi mjini hapa.
Maofisa wa Takukuru walilazimika kumkamata Jaji
Jonathan baada ya kukaidi wito wa taasisi hiyo uliomtaka kutoa maelezo
kuhusiana na uchunguzi wa shauri la kughushi nyaraka.
Jaji Jonathan ndiye aliyeandaa hati zinazoonyesha
mtoto wa miaka 15, Onass Edward Kyauka alikuwa ameuza kiwanja cha urithi
kwa Sh10 milioni kwa mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Edward
Eugen Mushi.
Hata hivyo, mtoto huyo ambaye wakati huo alikuwa
akisoma kidato cha pili, alikanusha kuwahi kufika mbele ya Jaji Jonathan
kusaini nyaraka zozote na kwamba, saini iliyokuwapo katika nyaraka hizo
haikuwa yake.
Tuhuma hizo ziliifanya Takukuru ifungue jalada la
uchunguzi na Jaji Jonathan aliitwa kuhojiwa lakini alikataa akidai kuwa
sheria inamlinda kutotoa siri za mteja wake.
Takukuru ililazimika kumkamata Juni 5, mwaka 2007.
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment