Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAUGUZI nchini wametakiwa kufahamu kuwa wao ni nguzo muhimu katika
sekta ya afya na kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu, ili waweze
kukumbukwa na jamii pindi watakapostaafu.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Timoth Wonanji, alipozungumza na Tanzania Daima kuhusu hali ya wauguzi katika halmashauri yake.
Alisema wauguzi wanapaswa kuleta mabadiliko katika sehemu zao za kazi
na kutumia nguvu walizonazo kuleta mabadiliko katika sekta hiyo pamoja
na kuhakikisha changamoto zinazosababishwa na wauguzi zinaondoka
kabisa.
“Unajua muuguzi ni nguzo kubwa katika sekta ya afya na wao ndio
watendaji wakubwa ukilinganisha na madaktari, hivyo wanapaswa kuacha
kitu ambacho kitakuwa kikikumbukwa kwa kufanya kazi kwa uaminifu na
uadilifu,” alisema.
Akijibu swali la tatizo la watumishi, mganga huyo alisema tatizo si
watumishi, bali ni utendaji kazi wa watumishi hao na kutoa mfano kuwa
unaweza ukawa na watumishi 100, lakini utendaji kazi wao ukawa ni
mbovu.
Alieleza kuwa suala la utendaji kazi bora ndiyo linalohitajika na si
kubaki kusema kuwa wana tatizo la upungufu wa watendaji katika sekta
hiyo na kufafanua kuwa wilaya yake haina tatizo la upungufu wa wauguzi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment