Home » » MAAMBUKIZI YA VVU YAONGEZEKKA MOSHI

MAAMBUKIZI YA VVU YAONGEZEKKA MOSHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

MAAMBUKIZI ya virusi vya ukimwi (VVU) katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro yameongezeka mara dufu kutoka asilimia 1.2 mwaka 2012 hadi asilimia 2.1 mwaka 2013.
Takwimu hizo zilitolewa na Mratibu wa Ukimwi wa halmashauri hiyo, Benedicto Rwamuhuru, wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu hali ya maambukizi ya VVU kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 wakati wa warsha kwa waandishi wa habari mkoani hapa.
Warsha hiyo ililenga kuwajengea waandishi uwezo wa kuandika na kutangaza habari zinazohusu maambukizi ya virusi hivyo na ukimwi.
Rwamuhuru alisema viwango vya maambukizi vimeongezeka mara dufu katika halmashauri hiyo yenye tarafa nne na kata 31, huku akieleza sababu za ongezeko hilo kuwa ni ulevi, ngono zembe, umasikini na mwingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kirua-vunjo mashariki, Jaffer Mbwambo, alisema maambukizi yanaenea kwenye kata hiyo kwa kuwa baadhi ya koo zinaendeleza utamaduni wa kurithi wajane.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa