Home » » MAHAKAMA YAVUNJA NDOA YA ASKOFU

MAHAKAMA YAVUNJA NDOA YA ASKOFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Mahakama ya Mwanzo ya Mjini Moshi, imevunja ndoa ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Furaha Tanzania (KLFT), Askofu Jones Molla na Liliani Dani Kimambo, iliyofungwa mwaka 1978 katika kanisa la Kipentekoste, lililopo Majengo, mjini hapa.
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi mwishoni mwa wiki, Askofu Molla na aliyekuwa mkewe, Liliani, walithibitisha kuvunjwa kwa ndoa yao.

Hata hivyo, Liliani, alisema hatambui uamuzi huo wa mahakama kwa kuwa ulitolewa kwa kusikiliza upande mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Liliani alisema ingawa talaka hiyo imetolewa, yeye binafsi hajawahi kuitwa mahakamani ili kutoa maelezo yake wakati wa shauri hilo.

"Askofu Molla bado ni Mume wangu halali wa ndoa, nina mpenda sana. Nyie waandishi muulizeni huyo Askofu Molla, mbona amekwenda kuoa mwanamke mzee kama mimi?, kwa nini

asioe msichana?...hiyo hainitishi na hakuna mahakamani inayovunja ndoa iliyounganishwa na Mungu," alisema.Kwa upande wake, Askofu Molla alisema ameachana na mkewe huyo

kutokana na fitina alizokuwa akizipokea kutoka kwa baadhi ya wachungaji wa kanisa la Kipentekoste na kuwa tangu mwaka 2009, mke aliondoka nyumbani na kwenda kuishi na wazazi wake kinyume na maandiko ya Mungu ambayo yanasema utaambatana na mume wako hadi kifo kitakapo watenganisha.

Hatua ya mahakama kuvunja ndoa hiyo imetolewa kufutia shauri la talaka namba 16/4/13 lililofunguliwa na Askofu Molla, akidai tangu mwaka 2009 mkewe Liliani alitoroka nyumbani na juhudi za kumrejesha zilikwama.

Kufuatia hali hiyo, Hakimu Mrisha, aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, alisema baada ya kusikiliza mgogoro wa ndoa hiyo na vielelezo vilivyopelekwa mbele yake kutoka Ustawi wa Jamii na kanisa lililofungisha ndoa hiyo, amejiridhisha kuwa wawili hao sio mke na mume tena kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971.

Kwa upande wake, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kipentekoste Majengo, James Rukate, amekiri kanisa lake kufungisha ndoa hiyo mwaka 78 na kuwa walipewa shahada namba  42335.

Kuhusiana na madai ya Askofu Molla kuwa wachungaji wa kanisa hilo ndiyo waliotia fitina hadi kupelekea kuachana na mkewe na kuhama kanisa hilo na kwenda katika kanisa jingine, Mchungaji Rukate alisema hilo hana uhakika nalo.

Wanandoa hao wametalaikiana wakiwa na watoto 10 na wajukuu saba.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa