Home » » TASO KUKUSANYA MIL.159/-MAONYESHO NANENANE

TASO KUKUSANYA MIL.159/-MAONYESHO NANENANE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

CHAMA cha Wakulima na Wafugaji Kanda ya Kaskazini (TASO)kinatarajia kukusanya jumla ya sh.159,650,000 kutokana na vyanzo mbalimbali katika maonyesho ya 21 ya wakulima na wafugaji ambayo yanatarajia kuanza mwezi ujao katika viwanja vya Themi Njiro.

Hayo yalisemwa na mweka hazina TASO kanda ya kaskazini Isidori Tarimo alipokuwa akiwasilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha kamati kuu ya maandalizi ya maonyesho ya Kilimo ya sherehe za wakulima Nane nane.

Aidha bajeti hiyo inatokana na maandalizi ya sherehe hizo za Nane nane ambapo mapato mbalimbali yatapatikana kupitia sherehe hizo ambazo hufanyika kila mwaka.

Aidha alisema kuwa ili kuweza kukidhi bajeti hiyo TASO inategema kukusanya sh.129,650,000 huku halimashauri zote 20 zikiombwa kuchangia kiasi cha sh.1,500,000 kila moja na kuleta jumla ya sh.30,000,000 ili kuweza kufikia lengo halisi la bajeti hiyo.

Alifafanua kuwa bajeti ya matumizi kwa mkwa 2014 yanategemewa kuwa kiasi cha sh.i 154,001,000 ambapo maeneo makubwa yatakuwa usafiri na usafirishaji wa sh.13,679,000 iwapo mgeni rasmi atakuwa kiongozi wa kitaifa.

Alitaja matumizi mengine kuwa ni pamoja na zawadi kwa washindi mbalimbali wa halmashauri za mikoa ambao wataweza kuzawadiwa kiasi cha sh.18,000,000 ikiwa wote wataweza kukidhi viwango vilivyowekwa.

Aliongeza kuwa ili kuweza kukamilisha mchakato wa ushindanishi wa mifugo kikanda kwa usafirishaji wa mifugo Dodoma TASO anaiomba halimashauri zitakazotoa washindi wa mifugo zisaidie gaharama hizo ili kufanikisha msafara wa kanda hiyo.

Naye katibu wa cha hicho Peter Ngasamiakwi alisema kuwa maandalizi ya maonyesho hayo yanaendelea vizuri na kwamba tayari makampuni na mashirika yapatayo 474 yamedhibitisha kushiriki maonesho hayo

1 comments:

Anonymous said...

natumai mtafikia lengo my dad. Hard work pays! #team Tarimo

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa