Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA cha Wakulima na
Wafugaji Kanda ya Kaskazini (TASO)kinatarajia kukusanya jumla ya
sh.159,650,000 kutokana na vyanzo mbalimbali katika maonyesho ya 21 ya
wakulima na wafugaji ambayo yanatarajia kuanza mwezi ujao katika viwanja
vya Themi Njiro.
Hayo yalisemwa na mweka
hazina TASO kanda ya kaskazini Isidori Tarimo alipokuwa akiwasilisha
taarifa hiyo kwenye kikao cha kamati kuu ya maandalizi ya maonyesho ya
Kilimo ya sherehe za wakulima Nane nane.
Aidha bajeti hiyo
inatokana na maandalizi ya sherehe hizo za Nane nane ambapo mapato
mbalimbali yatapatikana kupitia sherehe hizo ambazo hufanyika kila
mwaka.
Aidha alisema kuwa ili
kuweza kukidhi bajeti hiyo TASO inategema kukusanya sh.129,650,000 huku
halimashauri zote 20 zikiombwa kuchangia kiasi cha sh.1,500,000 kila
moja na kuleta jumla ya sh.30,000,000 ili kuweza kufikia lengo halisi la
bajeti hiyo.
Alifafanua kuwa bajeti
ya matumizi kwa mkwa 2014 yanategemewa kuwa kiasi cha sh.i 154,001,000
ambapo maeneo makubwa yatakuwa usafiri na usafirishaji wa sh.13,679,000
iwapo mgeni rasmi atakuwa kiongozi wa kitaifa.
Alitaja matumizi
mengine kuwa ni pamoja na zawadi kwa washindi mbalimbali wa halmashauri
za mikoa ambao wataweza kuzawadiwa kiasi cha sh.18,000,000 ikiwa wote
wataweza kukidhi viwango vilivyowekwa.
Aliongeza kuwa ili
kuweza kukamilisha mchakato wa ushindanishi wa mifugo kikanda kwa
usafirishaji wa mifugo Dodoma TASO anaiomba halimashauri zitakazotoa
washindi wa mifugo zisaidie gaharama hizo ili kufanikisha msafara wa
kanda hiyo.
Naye katibu wa cha
hicho Peter Ngasamiakwi alisema kuwa maandalizi ya maonyesho hayo
yanaendelea vizuri na kwamba tayari makampuni na mashirika yapatayo 474
yamedhibitisha kushiriki maonesho hayo
1 comments:
natumai mtafikia lengo my dad. Hard work pays! #team Tarimo
Post a Comment