Home » » VITENDO VYA UBAKAJI,KULAWITI TISHIO ROMBO

VITENDO VYA UBAKAJI,KULAWITI TISHIO ROMBO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 

VITENDO vya ubakaji, kulawiti na wanaume kuanza kufanya mapenzi ya jinsia moja hadi wanafumaniwa na wake zao vimeshamiri wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro na sasa uongozi wa halmashauri umelazimika kuingilia kati na kutaka kuwepo mikakati ya kumaliza tatizo hilo.

Kukithiri kwa vitendo hivyo kumewekwa wazi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judathadeus Mboya, wakati wa mkutano ulioandaliwa na Asasi ya Utetezi wa Haki za Binadamu na Utoaji wa Ushauri wa Kisheria ndani ya Jamii (AJISO).

“Kumeibuka vitendo vya watu kufanya mapenzi ya jinsia moja. Kuna matukio ya wanawake kuingia katika nyumba zao na kuwakuta wanaume wakijihusisha na mapenzi na wanaume wenzao...ni lazima jamii kuchukua hatua kuhakikisha tabia hiyo inatokomezwa,” alisema Mboya na kuongeza;

“Vitendo vya ndoa za jinsia moja yaani mwanaume kufanya mapenzi na mwanaume mwenzake havikuwepo katika wilaya ya Rombo, lakini leo si vitu vya ajabu, hivi tumekuwa watu wa lazima tubadilike na kuondokana na aibu hii ambayo ni mbaya sana,” alisema Mboya.

Mboya, pia alisema kuna vitendo vya kubakana kulawiti ambapo waathirika wakubwa wa vitendo hivyo ni watoto. Katika mkutano huo ambao uliandaliwa na AJISO kwa lengo la kuwatambulisha wasaidizi wa msaada wa kisheria waliopatiwa mafunzo na shirika hilo, Mkurugenzi huyo alisema kumekuwepo na matukio ya watoto kulawitiwa na kubakwa.

Alisema hata watoto wa jinsia moja wamekuwa wakijihusisha na masuala ya mapenzi, huku matukio hayo yakifanywa kuwa siri. “Hali hii ni udhalilishaji mkubwa katika jamii,” alisema Mboya na kuongeza kwa kutoa mfano:

“Hivi karibuni katika eneo la Mamsera wilayani hapa, kuna watoto 10 wa kiume wa shule za msingi, ambao walikuwa wanachezeana mchezo mchafu (kulawitiana) na mtoto mmoja ambaye alikuwa mdogo zaidi, aliathirika vibaya sana na taarifa zilifika ofisini na watoto wale walikamatwa, lakini yule aliyekuwa mkubwa aliyehusika kuwaumiza wenzake alikimbia na hadi sasa anatafutwa na polisi, hili ni jambo la hatari na aibu.”

Alisema, halmashauri hiyo pia itatoa elimu kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara, ili kuwapa uelewa na kuwawezesha kutoa taarifa za matukio ya ulawiti na ubakaji, hatua ambayo itasaidia kutokomeza vitendo hivyo katika wilaya hiyo.

Alisema Halmashauri hiyo pia itatoa elimu kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara, ili kuwapa uelewa na kuwawezesha kutoa taarifa za matukio ya ulawiti na ubakaji, hatua ambayo itasaidia kutokomeza vitendo hivyo katika wilaya hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na AJISO katika kipindi cha mwaka jana 2013 kulikuwa na matukio 115 ya ubakaji na kulawiti yaliyoripotiwa katika shirika hilo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Anthony Tesha, alisema jani linaloitwa isale limekuwa likitumika kuombea msamaha kwa kabila la Wachaga, limekuwa likitumika vibaya kwa baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo, na kuchangia kuongezeka kwa vitendo vya kikatili na udhalilishaji kwa watoto na wanawake.

Tesha alisema jani hilo la isale ambalo ni vigumu kulikosa kwenye shamba la watu wa kabila la Kichaga, limekuwa likitumika katika maeneo mengi ya wilaya hiyo kufunika maovu, kutokana na kutumika kwenda kuombea msamaha pindi panapotokea mtu kujihusisha na vitendo viovu ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto, hivyo kuwa kichocheo kikubwa cha kuendelea kwa vitendo hivyo katika jamii.

“Mtoto anabakwa au analawitiwa Rombo, mzazi unaletewa Sale unafunika uovu ule na kupoteza ushahidi kabisa, hii ni hatari sana katika jamii, kwani vitendo hivi bado vimeen delea kushika kasi katika wilaya hii na waathirika wakubwa ni watoto wetu ambao ndio wanategemewa kuja kulijenga taifa hili hapo baadaye,” alisema Tesha

Chanzo;Majira

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa