Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERA
ya kudhibiti mavazi yasiyoendana na maadili, yanayovaliwa na wanafunzi
wa vyuo vikuu hapa nchini, inaelezwa itakuwa muarobaini kwa wanafunzi
husika.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Mkuu wa Chuo Kikuu
Kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) cha Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine (SUA), Profesa Faustine Bee, alisema serikali ipo katika
mchakato wa kuanzisha sera hiyo ambayo wanaamini itakuwa msaada mkubwa
wa kulinda uvaaji vyuoni.
Alisema kuwa chuo hicho pamoja na vyuo vingine haviwezi kuwaruhusu
wanafunzi, hasa wa kike kuvaa mavazi ya nusu uchi yanayoshushia heshima
vyuo na utu wa wahusika.
Prof. Bee alisema kuwa pamoja na sera hiyo kuwa hatika hatua za
mwisho, walengwa ambao ni wanafunzi, nao watashirikishwa ili kutoa maoni
yao juu ya mfumo stahiki wa mavazi hayo na kuongeza wakubali wasikubali
sera hiyo ni mhimu kwa lengo la kudumisha heshima ndani ya jamii.
Alisema suala la nidhamu ni muhimu kwa lengo la kujenga maadili mema
ndani ya jamii na kuongeza kuwa vijana wengi wamejiunga na vyuo
wakitokea kwa wazazi wao, lakini wamekuwa na uhuru wanaoutumia vibaya.
Prof. Bee alisema kama vijana wataendelea kulelewa kwenye maadili mema, taifa litakuwa na kizazi chenye staha.
Kwa mujibu wa Prof. Bee, mchakato wa sera hiyo ya mavazi ukikamilika
utarasimishwa rasmi na mwanafunzi atakayeikiuka ataondolewa chuoni hapo.
Katika hatua nyingine, chuo hicho kimekaribisha wawekezaji
watakaojenga hosteli na sehemu za chakula kwa ajili ya kukidhi mahitaji
ya wanachuo na wafanyakazi wake
Chanzo:Tanzani Daima
0 comments:
Post a Comment