Home » » KORTI YAAMURU MAITI KUFUKULIWA

KORTI YAAMURU MAITI KUFUKULIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Korti yaamuru maiti kufukuliwaMGOGORO wa kugombea mwili wa marehemu, Stephen Assei (52) umechukua sura mpya baada ya askari polisi wenye silaha za moto wakiwemo askari kanzu kusimamia zoezi la ufukuaji wa kaburi na kisha kuondoka na jeneza lenye mwili wa marehemu.
Hatua ya ufukuaji wa kaburi hilo inatokana na mke wa ndoa wa marehemu, Lucy Laurant kufungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi dhidi ya Fortunata Lyimo, akidai shughuli za maziko za marehemu mumewe zifanyike nyumbani kwake kijiji cha Mandaka.
Lucy aliiomba mahakama hiyo kutoa amri ya kufukuliwa kwa mwili wa Marehemu, Assei aliyefariki Septemba Mosi mwaka huu na kuzikwa Agosti 8 mwaka huu katika kijiji cha Masaera kata Kilema Kusini nyumbani kwa mke wa pili wa marehemu aliyekuwa akiishi naye kwa zaidi ya miaka 18.
Ombi hilo lililowasilishwa na wakili wa upande wa mashitaka ,Paul Njau, mbele ya Hakimu Mkazi Munga Sabuni, iliamriwa kufukuliwa kwa kaburi hilo na mwili kuhifadhiwa hospatali hadi Septemba 11 mwaka huu mahakama itakapoamua ni nani mwenye haki ya kumzika marehemu.
Baada ya shughuli za kufukua kaburi kumalizika, jeneza lenye miwli wa marehemu lilipakizwa katika gari la Polisi ,Land Rover 110,lenye namba za usajili ,T 989 AEV na kupelekwa katika hosptali ya Kilema kwa ajili ya kusibiri uamuzi wa mahakama.
Baada kaburi kufukuliwa, ndugu wa marehemu wakiongozwa na kiongozi wa Ukoo aliyetambulika kwa jina la Basil Assei wamejitokeza na kumkana mlalamikaji anayetajwa kuwa ni mke wa ndoa wa marehemu.
“Marehemu akiwa mgonjwa alisema hataki kuzikwa katika mji wake wa zamani anataka kuzikwa katika mji huu aliojenga mwenyewe, halafu cha kushangaza zaidi hata watoto aliozaa na marehemu wanakaa kwa huyu mke mdogo,” alisema Basil.
Katika hali isiyo ya kawaida kaburi alilokuwa umezikwa mwili wamarehemu Assei, liliachwa wazi huku baadhi ya wananchi waliokuwawakishuhudia zoezi la ufukuaji wakisema kwa mila za kichaga kunahitajika kufanyika shughuli za kimila kabla siku haijaisha.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa