Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWANAHARAKATI na mdau wa maendeleo ya wananchi wa Same Mashariki,
Allan Mmanyi ‘Mkombozi’ amesema hali ya maisha ya wakazi wa vijiji vingi
vya Same Mashariki inasikitisha kwa kuwa wengi wao wamekata tamaa.
Mkombozi anayefuatilia kwa karibu maisha ya wananchi wa eneo hilo
mkoani Kilimanjaro, ameliambia gazeti hili kuwa kila siku watu wa Same
Mashariki hushukuru Mungu kwa kusema afadhali ya jana kwani, kilimo kama
nguzo kuu ya kiuchumi kwao, kimekuwa hakiwaletei tija yoyote.
“Ni hatari ukifika vijiji vya Vuje, Maore, Ndungu, Bombo, Mvaha na
milimani ukawauliza wakulima wanachohitaji utawasikia wakilalamika shida
yao ni ukosefu wa soko la uhakika la mazao na uhaba wa pembejeo.
“Hawajui nani atawajibika kuwalipa japo fidia kidogo ya hasara
waliyopata. Kwa kweli ni ukatili uliopitiliza ambao watu wa Gonja
milimani wanafanyiwa… upande wa elimu, ni shida shule chache, walimu
hawatoshi, maabara hakuna huku umbali ukiwa kikwazo kwa wanafunzi wa
baadhi ya maeneo," alisema.
Alisema anajipanga kufanya mapinzudi ya kilimo na kwamba ameandaa
mpango wa kuwawezesha wana Same Mashariki kuepukana na adha hiyo kwa
kubuni njia mbadala za kilimo chenye tija.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment