Home » » WAZURU KIWANDA CHA KIMEA MOSHI

WAZURU KIWANDA CHA KIMEA MOSHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

VIONGOZI wa Vyama vya Ushirika mkoani Arusha, wamefanya ziara kiwanda cha kimea kinachomilikiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na kuonesha kufurahishwa na namna kimea kinavyoandaliwa hadi kuwa bia.
Ziara hiyo iliyofanyika hivi karibuni, inaelezwa kuwa ni sehemu ya mafunzo kwa wakulima ili kuwawezesha kulima Shayiri iliyo bora na safi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kiwandani hapo, Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Monduli Juu, Barrick Kivuyo, aliishukuru TBL kwa kuendelea kuwajali na kuwapa mafunzo yanayolenga kuboresha zaidi kilimo cha Shayiri kwa wakulima wa ndani.
“Tumetembelea kiwanda cha kuzalisha kimea cha Moshi ili tujifunze namna bora ambayo itatuwezesha wakulima kuiandaa Shayiri huko shambani katika mazingira safi, kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, hadi kuvuna,” alisema.
Naye Meneja wa Kiwanda hicho, Vitus Mhusi, alisema ziara hiyo italeta mafanikio zaidi katika msimu ujao.
chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa