WADAU wa elimu nchini wameilaumu serikali kwa kubadilisha mara kwa
mara viwango vya ufaulu bila kufanya tathimini ya kutosha, mpango
uliofananishwa na upanuzi wa magoli ili kumwezesha kila mchezaji
kufunga kirahisi.
Lawama hizo zilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Shule ya Sekondari
Majengo iliyo chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Peter Lyimo,
katika hotuba yake kwenye mahafali ya 28 ya wahitimu 568 wa kidato cha
nne.
Alisema kuwa, hali hiyo ni ya hatari na inaua elimu na taifa haliwezi
kuendelea kwa mfumo huo na kushauri serikali kuiboresha elimu ili
iweze kuandaa wanafunzi kuweza kujitegemea.
Aliitaka serikali kuziboresha shule za ufundi na kuzipa msukumo wa
pekee, akiamini kuwa ni muhimu kwani zinawezesha kuzalisha kazi badala
ya kufatufa kazi.
Mkuu huyo shule, alisema elimu ya Tanzania haiwezi kuwa bora kama
wananchi hawataimiliki kwa mchango na uwajibikaji na kuongeza kuwa,
kama taifa na jamii yanahitajika mabadiliko ya kifikra na kimtazamo
kuhusu elimu.
“Ndugu zangu, tunatakiwa kuchangia elimu yetu ili iwe bora, kuna
wanafunzi wengi ambao wanashindwa kusoma kutokana na kukosa msaada,
tunakumbuka kwamba kila mmoja wetu hapa amefika alipo kwa kutembea
mgongoni mwa mtu mwingine…baba, mama, mjomba, shangazi na wengineo,”
alisema.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment