Home » » DIWANI TLP AMSALITI MREMA, AJIUNGA UKAWA

DIWANI TLP AMSALITI MREMA, AJIUNGA UKAWA

LICHA ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema kutangaza mara kadhaa kutounga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), diwani wa chama chake katika Kata ya Mwika Kusini, Meja mstaafu Jesse Makundi, amesema anakubaliana na umoja huo.
Makundi alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, na Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia katika vijiji vya Maring’a na Mrimbo, Uwoo, Moshi Vijijini ili kuwanadi wagombea wa vyama vinavyounda umoja huo.
Diwani Makundi ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa zamani wa jimbo hilo na Katibu Mkuu wa TLP Taifa, alijitokeza katika mikutano ya Mbatia huku akishiriki katika kuwanadi wagombea wa Chama cha NCCR-Mageuzi.
“Ndugu zangu wakazi wa maeneo ya Mrimbo-Uwoo na Maring’a msimshangae kwa kuamua kuandaa na kushiriki mikutano ya Ukawa pamoja na kumuunga mkono mbunge wa Mbatia kwa sababu yeye ni kiongozi wa wananchi wote wakiwamo wa CCM na vyama vingine,” alisema Mbatia.
Chanzo;Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa