Home » » KINANA AWATAKA VIONGOZI WEZI, MAFISADI KUNG'OKA HARAKA CCM‏

KINANA AWATAKA VIONGOZI WEZI, MAFISADI KUNG'OKA HARAKA CCM‏


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake ukiwa umezingirwa na wananchi wa jamii ya kimasai ulipokuwa ukiondoka baada ya kuhutubia mkutano katika Kijiji cha Mtakuja, Kata ya Kia, Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro leo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Kinana ambaye katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Itikadiu na Uenezi, Nape Nnauye, ameutaka uongozi wa Kampuni ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kuacha kuwabughudhi wananchi wa kata hiyo, baada ya kutoa mallamiko kuwa unataka kuwapora ardhi iliyo karibu na uwanja huo yenye ukubwa wa zaidi ya hekali 10,000 inayomilikiwa na vijiji 11.

Komredi Kinana amekemea tabia hiyo ya baadhi ya viongozi wanaopora kinguvu ardhi za wananchi. Pia amewahakikishia wananchi hao kuwa atasaidia kurejesha ardhi hiyo kwa kukutana na Rfais Jnakaya Kikwete na kumwambia juu ya dhulma hiyo/

Komredi Kinana , amesema kuwa kiongozi yeyote aliyeingia CCM kwa minajiri ya kutaka kujineneemesha binafsi kimaisha, kwanzia sasa hatakuwa na nafasi na inabidi aondoke katika chama hicho ambacho kazi yake ni kutetea haki za wanyonge.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD  MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Komredi Kinana akishangiliwa na wananchi wa Kijiji hicho cha Mtakuja kinachokaliwa na jamii ya wamasai.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akishangiliwa na wananchi wa Kata ya Kia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtakuja.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Komredi Kinana.
 Wananchi wa Kata ya Kia, wakimpatia zawadi ya vazi la Kimasai pamoja na fimbo, Komredi Kinana wakati wa mkutano huo.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutao wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mtakuja, Kata ya Kia, Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara mjini Hai leo. Jimbo hilo linaongozwa na Mbynge, Freeman Mbowe wa Chadema. Amesema mbunge huyo ajiandae kuachia jimbo hilo kwani katika uchaguzi wa mwezi Oktoba CCM mwaka huu itashinda kwa kishindo na kutwaa jimbo hilo
 Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Komredi Kinana mjini Hai wakati wa mkutano wa hadhara.
 Waziri wa Elimu wa zamani, ambaye pia alikuwa waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Israel Nawinga, akimueleza jambo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipotembelewa na viongozi wa CCM kumjulia hali nyumbani kwake Losaa, Masama wilayani Hai leo.
 Komredi Kinana akishiriki kuchimba msingi wakati wa ujenzi mpya wa majengo ya Shule ya Msingi Modio iliyopatwa na jangoa la tetemeko na kubomoka eneo la Masama Mashariki, wilayani Hai.

 Watoto wanaosoma Shule ya Awali wakipita bila woga kwenye Daraja la zamani sana la Mnepo liliotengenezwa kwa kamba za waya katika Kijiji cha Kiyungi, wilayani Hai.
 Mmiliki wa Blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda akipita kwa uangalifu kwenye Daraja la zamani la Mnepo, wilayani Hai, Kilimanjaro leo.
 Komredi Kinana akishiriki kupaka rangialiposhiriki ujunzi wa daraja jipya la Mnepo lililojengwa kwa fedha za Serikali takribani sh. bilioni 1 katika Kijiji cha Kiyungi mpakani mwa wilaya za Hai na Moshi Vijijini.
 Komredi Kinana akikagua ujenzi wa Daraja jipya la Mnepo
 Komredi Kinana akipita kwenye daraja la zamani la Mnepo lililojengwa enzi za ukoloni katika Kijiji cha Kiyungi, mpakani mwa Wilaya za Hai na Moshi Vijijini. Daraja hilo limejengwa na kwa waya.
 Komredi Kinana akimkabidhi ng'ombe iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwa Kijiji cha Kwasadala kilichofanya vizuri katika uchaguzi uliopita hivyo kuipatia CCM ushindi mnono. Pia kijiji hicho kilikabidhiwa gunia moja la mchele.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Jimbo la Hai.
 Wananchi wakipiga picha za kumbukumbu wakati Komredi Kinana akihutubia katika Kijiji cha Mtakuja, Kata ya Kia, wilayani Hai.
 Komredi Kinana akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, ambapo pia alikagua ujenzi wa chumba kipya cha Xray, katika Mji wa Bomang'ombe, wilayani Hai.
 Komredi Kinana akiijaribu mitambo ya Xray iliyopo katika chumba hicho cha upimaji kwa njia ya mionzi.
 Nape akipigwa mionzi (Xray) ya mkono wake wa kulia
Wauguzi na watumishi wa hospitali ya Wilaya ya Hai, wakiwa katika picha ya pamoja na Komredi Kinana.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa