Home » » PROF.JUMANNE MAGHEMBE: SERIKALI IMEVALIA NJUGA TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI NCHINI‏

PROF.JUMANNE MAGHEMBE: SERIKALI IMEVALIA NJUGA TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI NCHINI‏


Akizungumzia tatizo la maji nchini kwa ujumla Prof. Maghembe amesema serikali iko katika utekelezaji wa miradi ya maji awamu ya pili ambapo serikali inatekeleza miradi ya maji katika miji mikuu mbalimbali hapa nchini, ambapo ifikapo mwaka 2025 upatikanaji wa maji katika miji mbalimbali kufikia asilimia 75% wakati katika jiji la Dar es salaam upatikanaji wa maji utafikia asilimia 95, hata hivyo Prof. Maghembe amongeza kwamba miradi hiyo inatekelezwa kwa gharama kubwa na serikali ina nia ya dhati ya kumaliza tatizo hilo nchini kwa kiwango kikubwa. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANGA KILIMANJARO) 2Mbunge wa jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji Mh. Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na wananchi katika kata ya Kileo ambapo alikagua ujenzi wa nyumba za walimu. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya sekondari ya Kileo wilayani Mwanga. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe wakikagua skimu ya umwagiliaji kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe wakishiriki ujenzi wa mifereji ya skimu ya umwagiliaji kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga. 6Wananchi wa Kijiji cha Kivulini wakitafakari jinsi ya kukwamua pikipiki yao ambayo ilikwama kwenye moja ya mifereji yenye tope katika skimu hiyo ya umwagiliaji. 8Nape Nnauye akijaribu kuendesha Skaveta mtambo wa kuvunia mpunga katika kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. 9Nape Nnauye akishuka kwenye Skaveta mtambo wa kuvunia mpunga katika kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. 10Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili katika kijiji cha Mangara Lembeni wilayani Mwanga. 11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe kushoto wakipiga makofi kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Mangara Lembeni wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. 12 Waziri Prof. Jumanne Maghembe akicheza ngoma ya asili ya wapare huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma hiyo wakati alipowasili katika moja na vijiji alivyotembelea na kuzungumza na wananchi wilayani Mwanga. 13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe wakishiriki ujenzi wa jengo la KKKT Mwaniko wilayani Mwanga 14Waziri wa maji na Mbunge wa jimbo la Mwanga Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga 15Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 16Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 18Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga. 19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo uliofanyika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa