Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Msaada wa magodoro uliotolewa na Benki ya NMB kwa waathirika wa mafuriko yaliyotkea hivi karibuni wilayani Hai.
|
Meneja
wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada wa kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni
ukanda wa chini wilayani Hai. |
|
Msaada wa magodoro uliotolewa na Benki ya NMB kwa waathirika wa mafuriko yaliyotkea hivi karibuni wilayani Hai. |
|
Meneja
wa NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akikabidhi msaada kwa mkuu wa
wilaya ya Hai, Anthony Mtaka huku zoezi hilo likishuhudiwa na mbunge wa
jimbo hilo Freeman Mbowe. |
|
DC Mtaka, Mbunge Mbowe na Meneaja wa NMB ,Bishubo wakifurahia msaada huo. |
|
Msaada mwingine uliotolewa ulikuwa ni wa Blankets. |
|
Chakula pia kilitolewa kwa wahanga hao. |
|
Meneja wa NMB,Vicky Bishubo akiwa na wahanga wa mafuriko .Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini
Benki ya NMB imetoa msaada wa
kibinadamu wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 10 baada ya kutembelea eneo la tukio na kujionea athari kubwa
zilizosababishwa na mafuriko hayo.
Akizungumza wakati wa kutoa
msaada huo Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo,alitoa pole
kwa familia zilizofikwa na kadhia hiyo huku akisema NMB imeguswa na
tukio hilo na kwamba inatoa msaada katika maeneo matatu.
Alisema eneo la kwanza la
msaada ni chakula ambapo imetoa unga kilo 2,000, Maharage Kilo
500,Sukari Kilo 500 na mafuta ya kula lita 1,000.
Eneo jingine ni eneo la malazi
ambapo yametolewa Magodoro 70,Mablangeti 100,pamoja na marobota ya nguo
huku pia Benki hiyo ikichangia mifuko 50 ya Sementi kwa ajili ya
ukarabati wa shule ya msingi Elerai iliyofikwa pia na mafuriko
“Tumesikitishwa na majanga
yaliowakuta,NMB tumekuwa na desturi ya kurudisha faida yetu katika jamii
kwa kusaidia majanga mbalimbali hivyo tumetoa msaada wa vifaa
mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 10”alisema Bishubo
Nao baadhi ya wahanga wa
mafuriko hayo waliishukuru NMB kwa msaada huo na kutoa rai kwa
watu,mashirika na taasisi mbalimbali zilizo za kiserikali na zisizo za
serikali kuona umuhimu wa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ya
kibinadamu kutokana athari zilizowakumba. |
0 comments:
Post a Comment