Home » » WANANCHI MANISPAA YA MOSHI WAALIKWA KUTOA MAONI JUU YA OMBI LA MUWSA KUBADILI BEI YA KUTOA HUDUMA YA MAJI.‏

WANANCHI MANISPAA YA MOSHI WAALIKWA KUTOA MAONI JUU YA OMBI LA MUWSA KUBADILI BEI YA KUTOA HUDUMA YA MAJI.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Dixon Busagaga.Moshi.

MAMLAKA ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) inakusudia kuongeza bei ya kutoa huduma za maji kwa watumiaji wake ,lengo likiwa ni kutaka kuendelea kufanya maboresho katika utolewaji wa huduma hiyo.

Kwa mujibu wa ombi Na,TR-W-15-008 kutoka Muwsa kwenda Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji(EWURA) Mamlaka ya maji safi na maji  taka mjini Moshi imetaka kuongeza beo ya huduma zake kwa mwaka 2015/2016 HADI 2017/2018.

Mabadiliko ya bei hiyo inayopendekezwa itawahusu makundi mbalimbali ya watumiaji wa huduma hiyo hususani wale wa majumbani,Taasisi,Biashara ,Viwanda na wale wa kwenye Vioski.

Mapendekezo mapya ya bei ya utolewaji wa huduma hiyo kutoka kiasi cha sh 495 kwa  Uniti moja ya ujazo wa maji ilivyo sasa hadi kufikia 710 katika kipindi cha mwaka 2015/2016 na kiasi cha sh  746 kipindi cha mwa 2016/2017 kwa wateja wa majumbani na taasisi.

Kwa upande wa Biashara ,Muwsa imependekeza bei ya huduma hiyo kuwa ni kiasi cha sh  839 kwa uniti moja kipindi cha 2015/2016,n ash 881 kipindi cha mwak 2016/2017 kutoka kiasi cha sh 585 katika ,kipindi cha mwa 2014/2015.

Eneo jingine ni kwa watumiaji wa viwandani ,ambao Muwsa imepndekeza bei ya huduma kuwa ni kiasi cha sh 947 katika kipindi cha mwaka 2015/2016 hadi kufikia kiasi cha sh 994 mwaka 2016/2017 kutoka 660 za sasa.

Nao wamiliki wa vioski  bei iliyopendekezwa ni kiasi cha sh 696 katika kipindi cha mwa 2015/2016 hadi kufikia 731 katika kipindi cha mwala 2016/2017 kutoka kiasi cha sh 485 bei ya sasa.

Kutokana na hali hiyo mamlaka ya udhibiti wa wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeandaa mkutano na wananchi wa manispaa ya Moshi ili kutoa maoni yao juu ya ongezeko la bei za huduma za maji .

Mkutano huo unatarajia kufanyika June 4 mwaka huu ,kuanzia majira ya saa 4 asubuhi , katika ukumbi wa Hindu Mandal uliopo jirani kabisa na kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha mjini Moshi.

Mgeni rasmi katika mkutano huo anatazamiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa