Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Vyombo
vya dola vya Tanzania vimefikishwa mbele ya Mahakama ya Afrika ya
Haki za Binadamu vikilalamikiwa kukiuka haki za binadamu wakati wa
kushughulikia wananchi.
Vyombo hivyo vimeshtakiwa mahakakani hapo na raia watano wa Kenya
waliohukumiwa miaka 30 kwa kosa la wizi wa kutumia silaha katika benki
ya NBC, tawi la Mwanga Kilimanjaro.
Wakili wa watuhumiwa hao, Donald Deya, aliwaambia majaji wa
mahakama hiyo kuwa washitakiwa waliteswa, na kupigwa wakati wakiwa
chini ya ulinzi na kusababisha wenzao wawili kupoteza maisha.
Deya, ambaye ni mtendaji mkuu wa Umoja wa Mawakili Barani
Afrika (PALU), aliiiambia mahakama kuwa washitakiwa waliteswa na
kupigwa wakati wakiwa chini ya ulinzi wa vyombo vya dola, jambo ambalo
ni kinyume cha sheria na kwamba hata walipolalamika hawakusikilizwa.
Wakili Deya aliiambia mahakama hiyo iliyokuwa imefurika
wasikilizaji iliyokuwa ikiongozwa na Naibu Rais wa Mahakama hiyo, Elisie
Tompson kutoka Nigeria kuwa washitakiwa wakiwa mahabusu taratibu mbali
mbali za kisheria zinazohusu uendeshaji wa kesi hio zilikiukwa na
madai yao ya uchelewashaji wa kesi na kuteswa hayakupewa uzito
uliostahiki wala hayakufanyiwa uchunguzi.
Naye wakili wa serikali, Nkasoi Sarakika, ameiambia mahakama
kuwa, madai ya watuhumiwa kupigwa na kuteswa hayana ukweli kwani
taratibu zote za haki zao zilizingatiwa na kuwa vifo vilivyotokea kwa
watuhumiwa wawili ni "vya kawaida".
Jaji Elisie Thomson aliahirisha shauri hilo ambalo sasa
linasubiri hukumu inayotarajiwa kutolewa baada ya miezi mitatu.
Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na watu ilianzishwa
mwaka 2006 nchini Adis Ababa na makao yake makuu kuhamishiwa
Arusha mwaka 2007, hivi sasa imeanza kuwa kimbilio la baadhi ya
wananchi wa Afrika wanaolalamika kuwa hawatendewi haki na serikali zao,
ndani au nje ya mahakama.
Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Agustino Ramadhani, alisema mahakama
hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya baadhi ya nchi
ambazo ndio ziliounda mahakama hiyo kuchelewa kutoipa ridhaa yao ya
masuala ya nchi zao kusikilizwa na mahakama hii.
Baadhi ya nchi hizo, kwa mujibu wa Jaji Ramadhani, ni uhaba wa
fedha na kusuasua kwa baadhi ya nchi kuridhia mikataba ya kuanzishwa
kwake.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment