Home » » MREMA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE

MREMA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
IMAG0392 (3)Mgombea ubunge jimbo la vunjo kupitia chama cha TLP Agustino Mrema (kushoto) akipokea fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la vunjo kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya moshi vijijini FOLGENCE MPONJI(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)


MGOMBEA ubunge jimbo la Vunjo na mwenyekiti wa chama cha TLP ,Agustino Lyatonga Mrema ametamba kuwa jimbo hilo ni mali yake na hayuko tayari kuona likichukuliwa na manyang’au aliodai wa Ukawa.
 
Mrema alitoa kauli hiyo wakati akiongea na mamia ya wafuasi wa chama hicho muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea kiti hicho katika ofisi cha halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini.
 
 Mrema alisema kuwa jimbo la vunjo ni mali yake na hayupo tayari kuliacha lichukuliwe na manyang’au wa ukawa  ambao alidai ni wanyang’anyi.
 
Alisema amelazimika kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo kutokana na maombi ya wananchi wa jimbo la vunjo wengi wao wakiwa wanawake ambao muda mwingi walikuwa wakimfuata nyumbani kwake wakimtaka agombee kutokana na rekodi nzuri aliyo watendea kipindi kilicho pita,
 
Hata hivyo alieleza kuwa propaganda zinazo enezwa na wapinzani wake wakidai kuwa yeye amezeeka na ni mgonjwa, nizakupuuzwa kwani kwa sasa yeye ana afya njema na anataka aitwe ‘bebi’ huku akionya kuwa wanao tumia sera ya uzee na ugonjwa kwa lengo la kumwangusha kamwe hawatafanikiwa kwani wananchi wa vunjo pamoja na mkewake ,Rose Mrema ndio wenye kujua utendaji wake wa kazi na hivyo hwahitaji  kuchaguliwa mtu mwingine.
 
“ Mengi yamesemwa kuwa mrema hagombei ni mzee ni mgonjwa hivi mkiniona mimi ni mzee jamani ,mimi ni bebi ,uzee mwisho Chalinze ,waliokuwa na wasiwasi eti sigombei .sasa nagombea afya yangu imeimarika na hao ukawa wataisoma namba mwaka huu”alitamba Mrema

Mrema alisema kuwa kazi aliyo ifanya katika kipindi chake cha ubunge inaonekana na amejipanga kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo wananufaika zaidi na juhudi zake kwakuwa amekuja na kasi mpya ya kuwaletea maendeleo na tayari amenunua gari la kusafirisha abiria  (coster) linalotumika katika jimbo hilo kusafirisha wakina mama wajawazito, shughuli za misiba pamoja na kubeba wananchi katika maeneo yao bila kuwatoza malipo yoyote  
,
Hata hivyo mremna anaonekana kukubalika zaidi na akina mama ambao walidai kuwa Mgombea huyo amekuwa akiwapigania akiwa bungeni ili wapatiwe mikopo ya bei nafuu pia amenunua gari la abilia kwa ajili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa