Home »
» BARAZA LA HALAMSHAURI YA WILAYA YA MOSHI LAMCHAGUA MICHAEL KILAWILA KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI.
BARAZA LA HALAMSHAURI YA WILAYA YA MOSHI LAMCHAGUA MICHAEL KILAWILA KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
|
Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,wakiwa ukumbini hapo kabla ya kuapishwa.
|
|
Wagombea
waliopitishwa na Chadema kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri
na Makamu Mwenyekiti wakiwa katika ukumbi wa halmashauri hiyo. |
|
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kabla ya kuapishwa. |
|
Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,wakiapishwa kuwa madiwani rasmi. |
|
Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri hiyo,Moris Makoyi akiwa katika kikao cha kwanza cha baraza hilo. |
|
Katibu
tawala wilaya ya Moshi,Remida Ibrahim akiongoza zoezi la upigaji kura
kwa ajili yakumpata Mwenyekiti na Makamu wake wa Halmashauri hiyo. |
|
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akiteta jambo na Diwani wa kata ya Kahe ,Rodrick Mmanyi wakati wa kikao cha baraza hilo. |
|
Mgombea
wa nafasi ya Mwenyekiti kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Joseph Chata
akiomba kura mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya
Moshi. |
|
Mgombea
wa nafasi ya Mwenyekiti kupitia chama cha Demokasia na Maendeleo
(Chadema) Michael Kilawila akijinadi mbele ya wajumbe wa baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Moshi akiomba kuchaguliwa kuogoza baraza
hilo. |
|
Mgombea
wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Sephen
Charles akiomba kura mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani wa
Halmashauri ya Moshi. |
|
Mgombea
wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kupitia chama cha Demokasia na Maendeleo
(Chadema) Exaud Mamuya akijinadi mbele ya wajumbe wa baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Moshi akiomba kuchaguliwa kuogoza baraza
hilo. |
|
Mgombea
wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kupitia chama cha NCCR -Mageuzi Gibrata
Riwa akijinadi mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya
Moshi akiomba kuchaguliwa kuogoza baraza hilo. |
|
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akipiga kura wakazi wa zoezi hilo. |
|
Wajumbe wakishiriki zoezi la upigaji kura. |
|
Diwani
wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava akimpongeza Diwani wa kata ya
Kindi,Michael Kilawila baada ya kutangazwa mshindi kwa kupigiwa kura 36 . |
|
Madiwani wakifurahia mara baada ya kuvaa joho rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa baraza hilo. |
|
Mwenyekiti
mpya wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila
akiongozana na Makamu wake ,Exaud Mamuya wakati wakiingia katika ukumbi
wa baraza hilo. |
|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akitoa muongozo wakati wa uzinduzi rasmi wa baraza hilo. |
|
Mwenyekiti
wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akitoa
hotuba yake ya kwanza wakati wa uzinduzi rasmi wa baraza hilo. |
|
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi. |
|
Mwenyekiti wa Halamshauri ,Michael Kilawila na Makamu wake ,Exaud Mamuya wakifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya (hayupo pichani). |
|
Katibu
tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Severine Kahitwa akitoa maelekezo
mbalimbali ya uendeshaji wa baraza hilo kwa Madiwani na uongozi mpya wa
baraza hilo. |
|
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akifuatilia . |
|
Menyekiti
wa Chadema wilaya ya Moshi vijijini Ekarist Kiwia pia alikuwa ni
miongoni mwa mashuhuda wa mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri. |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Michael Kilawila. |
|
Makamu Mwenyekiti wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Exaud Mamuya. |
|
Ndugu wa madiwani wakifurahia nje ya ukumbi wa Hlamshauri ya wilaya ya Moshi mara baada ya Madiwani kuapishwa.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kakskazini (0755659929). |
0 comments:
Post a Comment