Home » » Mtandaowa Tigo 4G LTE kupanuka hadi Moshi

Mtandaowa Tigo 4G LTE kupanuka hadi Moshi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa 4G mjini moshi pia  udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.


Moshi,Januari,2016- Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambayo inaongoza kwa kuendesha maisha ya kidijitali imetangaza mpango wake wakupanua huduma ya intaneti ya 4G hadi Moshi ifikapo Februari mwakahuu. Huduma hiyo ilizinduliwa kwanza  jijiniDar es Salaam  mwanzoni mwa mwaka jana na baadaye ilisambazwa kwenye mikoa ya Arusha, Tanga, Dodoma na Morogoro, kwa ufanisi na  hivyo kuufanya mtandao wa 4G kuwa mpana na wakasi nchini Tanzania.

Ikichukuliwa kama teknolojia nzuri ya hivi karibuni kwenye sekta Ya mawasiliano duniani isiyo na dosari katika kuifikia huduma ya intaneti, teknolojiaya 4G LTE inakasi takribani maratan ikilinganishwa na   teknolojiaya 3G Ambayo inatumiwa na watoaji wengine wahuduma hiyo kwenye soko la Tanzania.

Akizungumza kwenye mahoajiano maalum na vyombo vya habari kwenye ofisiza Tigo mjini Moshi pempezoni mwa uzinduzi rasmi wa mbio za kila mwaka za masafa za Kilimanjaro Marathon, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha alisema kusambazwa kwa mtandaowa 4G kuna fanyika ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo wa kuwapatia wateja wake huduma ya hali ya juu duniani ilikuwawezesha kuendesha  maisha ya kidijitali.

“Mpango wa kupanua mtandao wa Tigo wa 4G hadi Moshi  kwa mara nyingine umeonesha sio tu kwamba Tigo inaongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye soko, balipia  kujikita kwake Kuongeza kufikiwa kwa intaneti kwaWatanzania wengi kadri iwezekanavyo,”alisema Wanyancha  na kubainisha kuwa  kuwalengo kubwa la kampuni hiyo ya simu  ni kuhakikisha huduma hiyo inaenea nchi nzima  ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2016.
              
Akizungumziambioza Kilimanjaro Marathon ambazo Tigo ni mdhamini mwenza,Wanyancha alisema kwamba kama kampuni ya maisha ya kidijitali aTigo imeamua Kuwaunga mkono  wanamichezo wa umekwa wake  hapa nchini ilikuwasaidia kufikia malengo yao ya muda mrefu katika   maisha.Wanyancha alihitimisha kuwa tangu mwaka jana  Tigo ilishawekeza dolamilioni 120 kwa mwaka kwenye  upanuzi wa mtandao wake pamoja na kuboresha maeneo ya mitandao  ya 4G na 3G na mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza  idadi ya kufikiwa kwa huduma kwa wateja nchi nzima.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kilimanjaro Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa