Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Ramadhan Mungi akionesha Bunduki aoina ya
Short Gun iliyokamatwa ikiwa imefichwa katika tundu la Choo katika eneo
la Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Ramadhani Mungi akizungumza na
wanahabari kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mkoa wa
Kilimanjaro hivi karibuni.
Na Dixon Busagaga wa Globuu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
JESHI
la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wa watatu kwa tuhuma za
kuhusika na matukio mbalimbali likiwemo la mauaji pamoja na unyang’anyi
wa kutumia silaha yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana na
mwanzoni mwa mwaka huu.
Mbali
na watuhumiwa hao Polisi pia imefanikiwa kukamata Bunduki aina ya
shortgun (Pump Action) yenye namba 69901 ikiwa imefichwa katika tundu la
choo nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa hao eneo la Shirimatunda katika
manispaa ya Moshi.
Bunduki
hiyo pamoja na risasi tatu imetajwa kukodishwa na watuhumiwa na kisha
kutumika katika shughuli za kihalifu ikiwemo uporaji wa fedha katika
maeneo tofauti na mali huku ikihusishwa pia kufanya mauaji.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishina msaidizi wa Polisi, Ramadhani
Mungi alithibitisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na bunduki na kwamba
watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika.
“Katika
siku za mwisho wa Desemba mwaka jana na siku za mwanzoni za mwaka huu
,kulikuwa na wimbi la matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya
Short gun ambayo pia ilisababisha mauaji,tayari tumewakamata watu kadhaa
na jana (juzi) asubuhi tuliweza kuikama silaha aina ya Short
gun.”alisema Mungi.
Wakati
huo huo matukio ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto
yameendelea kushika kasi mkoani ambapo hivi karibuni mwanamke mmoja
(jina limehifadhiwa ) alikatwa matiti yote mawili baada ya kujinasua
katika jaribio la kubakwa.
Kamanda
wa Polisi mkoani hapa,Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo huku akimtaja mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo kuwa ni Anold
Josephate ambaye alitoweka na matiti hayo baada ya kuyaweka katika mfuko
wa plastiki.
Alisema
tukio jingine linalo ashiria kuongezeka kwa makosa ya unyanyasaji na
ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni tukio la juzi ambapo
mwanamke mmoja aliyfahamika kwa jina la Vailet Apiniel ameuawa baada ya
kunyongwa shingo.
“Siku
za karibuni hapa yamejitokeza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yanayo
uaibisha mkoa wetu,matukio ya ubakaji,matukio ya watu kutupa vitoto,haa
ni matukio mabaya na jana tu kuna mwanaume aitwaye Denis Shayo
alimnyonga mke wake”alisema Mungi.
Alisema
eneo hili linahitaji kutolewa elimu ya kutosha huku akizitaka taasisi
zinazojishughulisha na utetezi wa masuala ya kijinsia kushirikiana na
jeshi la polisi katika kupambana na matukio kama hayo.
0 comments:
Post a Comment